Saturday, May 31, 2008

WIKI HII

Youth Christian organization fellowship, which conduct prayer as youth Christian prayer network
Mtandao huu wa maombi ya vijana walio dhamilia kudhihilisha Nguvu za Mungu duniani

Hata ikawa mwisho wa siku saba neno la bwana likanijia kusema mwanadam nimekuweka kuwa mlinzi juu ya nyumba ya izraeli [eze 3:16 ]
Mambo ya kuombea

v Ombea watumishi wa Mungu ambao mungu anawatumia juu ya Taifa , Mungu awape mafunuo juu ya Taifa utulivu na unyenyekevu mkubwa, kataa roho za kujiona bora kuliko wengine , ombea familia zao , ndoa zao ,mafanikio ya kiuchumi, hata kama wametenda dhambi omba toba juu yao , hawa ni maaskofu , wachungaji ,na wainjilsti,
v Ombea huduma ya mana ,mtumishi Mwakasege, ombea huduma ya agape,mtumishi fenandusi, ombea huduma ya mama lwakatale, Nabii mwingila,pastor hiza ,newlife oustrich under egon falk,huduma ya ukwata, huduma ya new life band, new life ministry , scripture union na huduma zingine nyingi Mungu ametumia huduma hizi kuvuna maelfu ya watu zikabidhi mikononi mwa Mungu

Kwa sara zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatiu [ waefeso 6:18]

Basi kabla ya mambo yote nataka dua na sala na maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote [1timoth 2:1]
· Msogeze mbele za Mungu huyu dada aitwae mary ni mwanafunzi anaye soma kwa mateso makali kwa sababu ya kuathilika na ukimwi omba uponyaji na rehema za Mungu juu ya maisha yake anaishi mkoani Tanga fanya dua sara na maombi kwa ajili yake
· Msogeze mbele za Mungu huyu kaka aitwaye hebron anasoma chuo cha usafilishaji Dar Mungu afungue mrango wa ada kabla ya tar16 january si chini ya 2laki kw semister ya kwanza
· Ombea ndoa za watu walio okoka , kataa vurugu,mikosi ,omba hali nzuri za kiuchumi,kataa Roho ya matengano, panda upendo mpya , panda amani, utulivu, na hofu ya Mungu kwenye ndoa hizo
· Ombea vijana walioingia kwenye uchumba,Mungu awafanikishe, watunze utakatifu, mmoja asiwe jeraha kwa mwingine, omba safari njema mpaka siku ya ndoa,kataa mahusiano yanayosababisha vijana wengi watoke kwenye mpango wa Mungu
· Ombea mabinti waliojiingiza kwenye ukahaba tu kwa sababu ya kukosa msaada yaani ni yatima , au mafukara , hana msaada wowote , au vijana wakiume waliojiingiza kwenye uvutaji wa bangi , madawa ya kulevya, upolaji, ujambazi, na mambo mengineyo ambayo si ya haki mbele za Mungu, hawakupenda kufanya haya ila ni kwa sababu tu ya kukosa msaada wakafikili njia rahisi ni hiyo omba rehema za Mungu juu yao·

Kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihilishwa apate kuzivunja kazi za ibilisi [1yoh 3:8b]
kataa Roho za mauti juu ya nchi na juu ya afrika mashaliki ikiwa ni pamoja na makafara, roho za ajali , miripuko ya magonjwa,umwagaji wa Damu na matambiko yanayoendelezwa na baadhi ya makabila nchini kitu ambacho kinapelekea laana juu ya nchi amuru hizo kazi za adui kuvunjika
kumbuka na huu ndio ujasiri tulio nao kwake ya kuwa tukiomba kitu sawa sawa na mapenzi yake atusikia [2 yoh 5;14]

Baada ya maombi haya unaweza kutuambia nini Mungu kafanya ukiwa na ushuhuda mistari ya kututia Moyo, au vitu fulai umevipata toka kwaMungu, ombea huduma hii mikoa yote ya Tanzania na Afrika mashariki, ombea waombaji wote wa huduma hii kumbuka kumuombea coordinator Tuntufye Andrew.