Friday, May 30, 2008

UNAVYOWEZA KUEPUKA LAANA NA VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA

Ndugu yangu mpendwa ambaye Mungu amekupa neema ya kuweza kufuatilia mafundisho haya, ninakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu kristo, ninacho amini ni kuwa Roho mtakatifu ana kitu cha kufanya na maisha yako mara utakapokuwa ukiendelea kuufuatilia ujumbe huu, na pia utaweza kuwa msaada katika kuwavusha wengine ambao wamefungwa na ibilisi kwa namna moja au nyingine, yamkini hata pasipo ya wao kujua wako chini ya vifungo.
Ndugu msomaji unayefuatilia mafundisho haya si watu wengi leo wanaamini habari hizi za Laana, vifungo vya nguvu za giza, ikiwa ni pamoja na mambo ya uchawi na ushirikina, lakini pamoja na hayo yote bado ni wazi kabisa kuwa maelfu ya watu wamekuwa wakiishi maisha ya taabu na manyanyaso makali ya adui, sababu ikiwa ni Roho za giza zilizo wafunga na zinazofuatilia maisha ya wengi leo.

Na hii ndio sababu ya Yesu kuja duniani na kuitwa mkombozi, tena sehemu nyingine amejulikana kama mkombozi wa wanyonge, ikiwa na maana pia kuwa ni mkombozi wa walioonewa, walio kata tamaa, na wanaosumbuliwa na mateso ya ibilisi, wanaoishi maisha ya taabu na dhiki pamoja na maumivu yanayosababisha mateso makali, huzuni na vilio maishani, kumbuka hili ni la muhimu kwako kuwa Yesu hakuishia tu kutuokoa na dhambi zetu, isipokuwa pia alijishugulisha na kila jambo lililohusu maisha yetu, Afya zetu,mafanikio yetu,ikiwa ni pamoja na Roho zetu.
Na ndio sababu ukisoma katika ule waraka wa tatu ambao Paulo alikuwa akimuandikia Yohana {3 Yoh 1:2} anasema "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile Roho yako ifanikiwavyo"
Ndugu yangu mpendwa, ni wazi kuwa watu wengi leo wamefanikiwa sana katika mambo ya Rohoni lakini si katika Afya zao, wala katika maisha, na imefikia hatua kana kwamba tumefikiria kuwa Bwana Yesu alikuja kushugulikia Roho zetu tu, kitu ambacho si kweli, Mtume Paulo alitamani kama ingeeleweka kuwa Bwana Yesu hakuishia tu Rohoni isipokuwa pia alijishugulisha kwenye biashara, Ofisini, shambani, kwenye mifugo, masomoni,na kwingineko kote kufanikiwe.
Ndio sababu ukiusoma huu mstari kwenye tafsiri mojawapo ya kingereza utakuta lile neno ufanikiwe katika mambo yote limeandikwa hivi "you may prosper in every things" sasa neno "prosper’ ukiliangalia tafsiri yake "to prosper is to be successful and become rich" yaani kuwa unayefanikiwa na hatimaye kuwa Tajiri, tafsiri nyingine "to prosper is to grow and develop in healthy way" yaani ni kuendelea kukuwa na kuwa na Afya iliyo salama .
Sasa hii ndio iliyo msukuma mtume Paulo kuandika kwenye huu waraka kuwa ninapojitaabisha kuomba, au ninapojitaabisha kufunga , kuutafuta uso wa Mungu kwa ajili yenu siku zote malengo Yangu na shauku yangu, na kiu yangu huwa inakuwa ni juu yenu kwamba Mungu awafanikishe kwenye mambo yote, sasa utakuta baada ya neno mambo yote anasema na kuwa na afya yako nini maana yake, kitu alichotamani waelewe ni kuwa Mungu asingeishia tu kuwafanikisha katika mambo yote isipokuwa baada ya kufanikiwa katika maeneo mengine bado Afya zao pia ziwe Salama.
Na anaposema kama Roho yako ifanikiwavyo maana yake ni kuwa Rohoni kulikuwa na mafanikio tayari, ambayo hakuyatilia shaka hayo, na ndio sababu ikawa Rahisi kutoa mfano kwamba vivyo hivyo mnavyoendelea kufanikiwa Rohoni, ndio vivyo hivyo natamani mfanikiwe katika mambo yote, ikiwa ni pamoja na Afya zenu.

Ndugu yangu mpendwa unaye fuatilia mafundisho haya ni vizuri ukatambua hili kuwa inawezekana kabisa wewe kama mtoto wa Mungu kufanikiwa kimaisha, kuwa na Afya iliyo salama na ukiendelea kumuishia Mungu siku zote za maisha yako hatimaye kuurithi uzima wa milele.
Na ndio sababu basi "tunaokolewa roho zetu, nafsi zetu, na miili yetu" Hii ndiyo iliyomlazimu Bwana Yesu kushuka kuzimu na kumpokonya shetani funguo za mauti ili aje atutangazie ushindi katika mambo yote tena hata dhidi ya mauti. Hivyo basi kilicho mfanya Bwana Yesu aje Duniani ni kutuokoa, na kutukomboa.
Ndugu msomaji kama Yesu alikuja kutuokoa au kutukomboa, hii ina maana kuna mahali tulikuwa mateka, au kunasehemu tulikuwa tumefungwa, na ndio sababu watu wengi leo wanaishi maisha ya taabu, vilio, kutofanikiwa ikiwa ni pamoja na manyanyaso ya Ibilisi sababu kubwa ikiwa ni vifungo na manyanyaso ya adui kitu kilichomfanya Bwana Yesu aingilie kati pale msalabani.
Hivyo basi ni muhimu ukalielewa hili kuwa Biblia inaposema Yesu alikuja kutuokoa ina maana kuwa kuna mahali ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe kama nguvu ya Bwana Yesu haikuingilia kati.
Na Bwana Yesu aliidhihilisha hii yeye mwenyewe alipokifungua kitabu cha nabii Isaya maana alizungumza maneno ya matumaini kwa ajili ya kuwafungua watu waliofungwa na kuwaweka huru wanaoteswa na kuonewa na nguvu za ibilisi. .
{Isaya 61:1-2 } "Roho ya Bwana Mungu i juu yangu Kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma Ili kuwaganga walio vunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao; kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao."
Ni muhimu ukafahamu kuwa Biblia inapozungumzia habari ya kuwatangazia mateka uhuru wao hii ina maana kuwa kuna maelfu ya watu wametekwa na ibilisi kiasi ambacho hawawezi kuponyoka huko kabisa mpaka imetokea nguvu fulani kubwa zaidi ya kuwatoa huko, ambayo si nyingeneyo yoyote isipokuwa ya Bwana Yesu


Jambo muhimu,
Ningependa ufahamu kwamba pamoja na kuwa roho za giza zinasababisha; magonjwa, vilio, mauti, kutokufanikiwa, mateso makali na mengineyo mengi
Roho hizi pia zinasababisha watu waishi maisha ya dhambi, na wengi wao huja kupata ujasiri wa kuacha mambo mabaya waliyokuwa wakifanya hapo awali tu baada ya maombi ya ukombozi, na ndio sababu kuna roho kama za uzinzi,uasherati na ushirikina na zinazofanana na hizi, amabazo kama mtu anazo huwa hawezi kuacha tabia hiyo kwa kushauriwa, kuwekewa kikao cha ndugu na ukoo, kupewa adhabu kali, au kwa kuwekewa ulinzi mkali, hizi njia zote haziwezi kusaidia kwa sababu kuna Roho iko ndani yake ambayo ndiyo inayo mshurutisha mtu huyu kufanya hayo anayo yafanya.
Nilipata kusikia habali za kaka ambaye alikuwa anatozwa faini mpaka laki tano kwa sababu ametembea na wanafunzi wa sekondari, na jinsi ambavyo faini hiyo bado haikuweza kusaidia. Pamoja na kuwa ni pesa kubwa, sasa unafikiri ni kwa nini faini kubwa namna hii haikuweza kusaidia, sababu ni kuwa kilicho hitaji kushugulikiwa ni ile roho tu ya adui iliyokuweko kule ndani ya yule kaka. na si vinginevyo.
Mateka wa ibilisi huwa anatengenezewa kiu ya kufanya dhambi kama vile wewe unavyosikia kiu ya kunywa maji, kwa maana hiyo basi huwa hawezi kuwa na amani mpaka amefanya hiyo dhambi.
Mateka wakati wote hufanya anacho shurutishwa kufanya na pia huwa hana maamuzi yake mwenyewe na ndio sababu sehemu nyingine Biblia ikasema "wana macho lakini hawaoni wana masikio lakini hawasikii," sasa basi sababu kubwa huwa inatokana na kuwa mateka wa Ibilisi, maana wakati huo mtu huwa haoni ubaya wa kitu anachokifanya. Isipokuwa anapokuja kukombolewa ndio anaanza kujutia na kuona alikuwa anatenda dhambi, na anaanza kutambua madhara.
Nakumbuka baada ya kufundisha somo hili la ukombozi kwenye mji Fulani, Dada mmoja alikuja mbele akapiga magoti akalia sana kiasi kwamba ilinibidi kufuatilia nini kilikuwa tatizo, nilipopata nafasi ya kuongea na yule Dada akanieleza kwa machozi huku akilia sana kuwa alikuwa ametoka kutoa mimba mda si mrefu, na jinsi ambavyo haikuwa inamsumbua kiasi kwamba aliweza kuwa na ujasiri hata wa kuongoza baadhi ya vipindi kanisani kama kusifu na kuabudu kwa kiingereza tunaita {praise and worship}
Akaniambia, ulipokuwa unaendelea kufundisha nimesikia kuhukumiwa isivyo kawaida naona dhambi yangu inakuja mbele yangu naomba Yesu anisamehe akaendelea kulia sana, na akanieleza jinsi ambavyo kesho yake alikuwa anatakiwa akaongoze {praise and worship} kusifu na kuabudu kanisani kwao na jinsi ambavyo isingemletea shida.kama asingekuwa amekutana na Bwana Yesu saa hiyo, maana siku hiyo ilikuwa ni jumamosi.
Kitu nataka uone kwenye ushuhuda huu ni hiki kuwa unaweza ukawa mateka wa ibilisi na bado uko kanisani, na bado unafanya baadhi ya huduma.
Hebu tuangalie mstari huu "Na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao"
Ndugu msomaji, Biblia inapoelezea watu kufungwa, na juu ya ukombozi unaopatikana kwa njia ya Yesu kristo, hii ina maana vifungo hivyo ni vya ibilisi, na kama ni vya ibilisi basi viko chini ya utawala wa nguvu za giza, majeshi ya pepo wabaya ikiwa ni pamoja na mambo ya uchawi na ushirikina,
Hivyo basi Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii Ina maana wako watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Sasa ukifuatilia tafsiri ya kiingereza ule mstari unao sema na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao utakuta anasema "and openining of the prison to those who are bound" maana yake ni kuwafungua vifungoni waliofungwa au kuwatoa magerezani waliofungwa, {wamefungwa wapi?} Kwenye magereza ya ulimwengu wa roho.{wamefungwa na nani} na Ibilisi.
Nini maana ya maisha ya vifungo au maisha ya kuwa gerezani
Maisha ya vifungo au maisha ya kuwa gerezani ni maisha ambayo mtu huwa anaishi kinyume cha neno la Bwana, ni rahisi kuishi maisha ya dhambi hata kama wakati mwingine huwa hapendi, hakuna kufanikiwa katika kila unalolifanya, ukifanikiwa hakuna amani, maisha yaliyotawaliwa na huzuni, ikiwa ni pamoja na mateso makali hakuna kusonga mbele kila siku kuwa kwenye eneo moja la maisha, kuwa na maisha yasiyo na tumaini, maisha yasiyo na furaha,
Hivyo basi maana halisi ya vifungo vya nguvu za giza ni kuwa huwa kunakuwa na roho za giza ambazo zinakuwa zimeshikilia maeneo fulani ya maisha yako, na kila siku hizi roho huwa zinakuwa ziko kazini kuhakikisha zinakuweka katika hali ya shida kutofanikiwa kiuchumi, kutokufanikiwa kiafya, wala katika jambo lolote unalohitaji kulifanikisha.
Wako watu ambao kila anapokaribia mafanikio Fulani ndio tatizo linakuja kutokea na kukwamisha mpango mzima wa mafanikio uliokuwa mbele yake lakini pia wapo watu ambao wakipata pesa tu. Au kazi Fulani ambayo ingemuingizia kipato, ndio matatizo yanatokea kwa mfululizo kiasi kwamba hawezi kufurahia tena mafanikio aliyoyapata sasa haya yote husababishwa na Roho za giza ambazo zinakuwepo kwa ajili ya kuhakikisha huyu mtu hufanikiwi.
Unaweza ukajiuliza swali hili,{Je ninaweza nikaamua leo kuondokana na vifungo hivi ?} Jibu Ndio; inawezekana kabisa maana hii ndiyo sababu iliyomfanya Bwana Yesu kuja hapa Duniani atuokoe na kutukomboa. Endelea kufuatana nami katika mfululizo huu}







Je nguvu za giza zipo?
wapo watu wachache ambao huwa hawaamini habari za utendaji wa nguvu za giza,. na wengine huamini kuwa wakisha okoka hawahusiki tena, na mambo yanayohusu nguvu za giza kitu ambacho si kweli, Je umeshawahi kujiuliza kwa nini Bwana Yesu kabla hajaondoka alituombea maombi haya Yoh 17 : 15 ‘Mimi siombi kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu’ ikiwa Bwana Yesu aliomba tulindwe na yule mwovu, hii inamaana kuwa alijua fika utendaji wa ibilisi na jinsi amabavyo maisha yetu yalihitaji ulinzi wa Mungu usiku na mchana. Na ndio sababu ukisoma ule mstari wa 12 ‘a’ anasema ‘nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa nikawatunza,,,,,’ unaweza ukaona jinsi ambavyo Bwana Yesu aliona umuhimu wa sisi kutunzwa, au kulindwa na ndio sababu alipokuwa akiondoka akaomba kwamba tulindwe na yule mwovu, hii ina maana kuwa alikuwa akitambua fika vifungo na manyanyaso ya Adui ambayo yalikuwepo ulimwenguni na ukiendelea kusoma ule mstari wa ‘20’ utakuta akiwaombea na wengine watakao amini au watakao okoka baadae yaani wewe na mimi tulioamini leo hii.na wengine wanao endelea kuamini anaseama ‘Wala si hao tu ninao waombea ;lakini na wale watakao amini kwa sababu ya neno lao’
Ukisoma katika ‘ Waefeso 6 :12’ anasema ‘kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama ;bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho’ Mtume paulo alipokuwa akiandika walaka huu alitaka tufahamu kuwa kushindana kwatu, au kwa tafsiri nyingine tungeweza kusema kupambana kwetu si kwa vita za mwilini isipokuwa ni juu ya falme na mamlaka za giza, moja ya tafsiri za kiingereza imetafsili hivi ‘against powers’ maana yake dhidi ya nguvu mbalimbali za kuzimu falme za nguvu za giza inaweza kuwa na maana {Utawala wa ibilisi ambao chini yake kuna mapepo, majini pamoja na na vinyamukela vya kuzimu } huko ndiko tunakotakiwa kupeleka mashambulizi yatu, tena akaendelea kusema juu ya wakuu wa giza hili maana yake watawala wa giza { ambao ni wachawi, washirikina, na waganga wa kienyeji } akaendelea kuelezea jinsi amabvyo tunatakiwa kupambana dhidi ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Sasa akisema majeshi ya pepo wabaya uelewe hivyo hivyo majeshi maana kuna maelfu na maelfu ya mapepo ambayo yanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha yanavuruga mipango mizuri ya Mungu kwenye maisha ya watu
Sasa hii inaweza kukupa kuwa na hakika kuwa nguvu za giza zipo na kuwa unahitaji kujipanga kwa maombi kila wakati ili kukabiliana nazo.
`
Hivyo basi ni muhimu kuamini tu kuwa nguvu za giza zipo na zina nguvu na kuwa zinatenda kazi Duniani mchana na usiku na hii sasa ndio sababu kuna vitu vinaitwa [vifungo vya nguvu za giza} {maagano ya mizimu} mambo ya uchawi na ushirikina, watu kuhangaika na mambo ya kuagua ,kutambika mizimu, ibada za wafu, na mengineyo mengi
Na mambo haya ndiy’o yanayosababisha maisha ya vifungo kwenye maisha ya watu wengi
Nakumbuka nikiwa na fanya huduma ya ukombozi katika mkoa fulani na Dada mmoja aliyekuwa amepagawa na roho za giza, tukiwa katika maombi zile roho za giza zilianza kupiga kelele zikieleza ‘Mama yake alitukabidhi huyu tumtunze alipozaliwa , tumemuoa, ni mke wetu, huwa tunakuja saa nane usiku tunafanya nae tendo la ndoa, hatuwezi kumuacha tumetoka nae mbali {yaani hujawahi kuona roho za giza zikilia kwa uchungu na kumngangania mtu,} haikuwa rahisi sana maana huyu Dada alikuwa chini ya mikataba mikubwa ya nguvu za giza, alikabidhiwa na mama yake pasipo ya mama yake kujua, Asante kwa Yesu aliyetupa mamlaka yote Mbinguni na Duniani maana kwa jina lake yule binti alifunguliwa, ndugu unayefuatilia mafundisho haya tunapoendelea na mafundisho haya utazidi kujua namna watu wanavyoingia kwenye vifungo na jinsi unavyoweza kumuingiza mwingine pasipo ya wao kujua.
----Siku moja mara baada ya kufundisha somo hili katika kongamano la wanafunzi wa sekondari na vyuo Dada mmoja alinieleza jinsi alivyoanza kumpenda sana kaka fulani bila hata ya yeye kujua kwa nini alimpenda kiasi kile, anasema gafra alikuwa hawezi tena kusoma na kuelewa darasani, kiasi kwamba angekuwa teyari kufanya jambo lolote ambalo yule kaka angeamua walifanye, nikamuuliza kama aliwahi kuwa na urafi wowote na yule kaka akasema hapana isipokuwa siku moja walikutana kwenye kongamano fulani la vijana yule kaka alimsalimia yule Dada, na aliposalimiwa anasema hakukuwa na kitu chochote kilichotokea na kuwa hakuwahi kumfikili huyu kaka ila anasema, siku moja kuna nguvu ilimshukia gafra, akajikuta anamkumbuka sana na kumpenda isivyo kawaida ndipo nikamuuliza kama baada ya pale kuna kitu chocho aliwahi kupokea kwa yule kaka ndipo makasema kuna siku tu nilisha ngaa maana aliniletea picha yangu ambayo inaonyesha alinipiga ila sikumbuki alinipiga wapi nilipoipokea tu ndipo hali ilipozidi kuwa mabaya zaidi na baada kuichukua ile picha nilianza kuumwa na kitovu kwa nguvu, hii ni sehemu tu ya ushuhuda kitu nilitamani ukifahamu ni kuwa kama hutatambua kujifunika katiaka ulinzi wa Bwana Yesu kila wakati na kila mahali ni rahisi tu kukamatwa, baadae tukatambua kuwa huyu kaka alipiga hii picha bila huyu Dada kujua na kuipeleka kwa wakuu wa giza ili aweze kumpata kwa kutumia madawa maana yule bint alionekana kuwa na misimamo Ashukuliwe yesu aliye mfungua binti huyu
Kumbuka hili siku zote jitahidi kukaa mkao wa kujilinda kila wakati maana unahitaji msaada wa Mungu siku zote usiku na mchana Biblia imesema wazi kabisa 1yoh 5 :18 ‘twajua ya kuwa kila aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda’ wala yule mwovu hamgusi.
Ni muhimu ukafahamu kuwa unahitaji kujilinda kwa maombi kwa kulisoma neno kwa kukaa makao wa kumuhofu Mungu kila wakati hii itamfanya adui asipate nafasi kwenye maisha yako na ndio sababu Biblia ikasema Yakobo 4 :7 ‘Basi mtiini Mungu. mpingeni Shetani, nae atawakimbia ninyi’ sasa basi kule kumtii Mungu, kutembea na hofu ya Mungu ndiko kunakokutengenezea imani na ujasiri wa kumpinga shetani kwenye eneo lolote la maisha yako nae akukimbie, maana watu wengi leo wameishi maisha ya vifungo tu kwa sababu ya utumwa wa dhambi, na ndio sababu Biblia ikasema 1yoh 5 :14 ‘Na huu ndio ujasiri tulionao kwake ya kuwa tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake,atusikia,,,,,,’ sasa waweza kujiuliza swali kuwa ni kwa nini akaanza na huu ndio ujasiri tulionao kwake, hii ina maana ya kuwa huwezi ukawa na ujasiri wa kusimamia Nguvu za Mungu katika kumpinga ibilisi kama hauja kaa kwa Mungu kwa miguu yote miwili



JE MTU ALIYEOKOKA ANAWEZA AKAVAMIWA NA ROHO ZA GIZA ??? NA HATA KUWA CHINI YA VIFUNGO, NA INAWEZEKANAJE NA HALI YESU ALIMALIZA YOTE MSALABANI.
Ndugu mpendwa unayefuatilia mafundisho haya, kila mahali ambako Mungu amenipa neema ya kufundisha masomo haya ya ukombozi nimekuwa nikiulizwa hili swali.na inawezekana hata wewe unashauku ya kujua mengi kuhusiana na hili,
Mpendwa unayefuatilia mafundisho haya, ni kweli kabisa kuwa hata mtu aliyeokoka anaweza akavamiwa na roho za giza.
Na zika athiri mambo yake, kama biashara yake, uchumi wake, ndoa yake na hata maisha yake kwa ujumla na bado akawa anaenda kanisani, anaomba, anaimba, na kufanya baadhi ya mambo,
Kumbuka adui mkubwa wa ibilisi ni yule aliyempokea kristo, na ndio maana wakati mwingine kuokoka kumetamkwa kama kutangaza vita, mtu aliyeokoka anafananishwa na mtu ambae yuko vitani na kuwa amezungukwa na maadui kila mahali, na kila adui anatamani kama angelimmaliza yeye maana anasababisha matatizo makubwa kwenye ufalme wa adui bila ya yeye kujua.
Watu wengi kwa sababu ya kutokuyasoma maandiko hudhani ya kwamba kuokoka ni kumaliza kila kitu ikiwa ni pamoja na uhakika wa kufika mbinguni na kumbe kuokoka ni kuanza safari ya maisha mapya katika ulimwengu wa mapambano, na ndio sababu Biblia ikasema katika 2kor 10 :12 kwamba ‘kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke, sasa ukiufuatilia huu mstari utagundua Biblia inatutaka tuwe waangalifu, maana Adui ni kama simba aungurumae anaye tafuta mtu apate kummeza, wakati huo huo ukisoma Yakob 4 :7 utakuta anasema ‘basi mtiini Mungu mpingeni shetani nae atawakimbia’ sasa kwa nini Biblia inakutaka umpinge shetani ndipo nakukimbie, hii ina maana usipompinga atakukimbilia wewe.
Ulinzi wa Mungu unakuwa juu ya mtu, tu pale anapokuwa Hodari katika Bwana huku akiutafuta uweza na nguvu zake, Efeso 6 :10 ‘Hatimae mpate kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake’
Nini maana ya kuwa hodari katika Bwana, huku ni kukaa kwenye maombi, kuwa na neno la Mungu ndani yako, kujifunza kuutafuta uso wa Mungu kwenye maeneo Mbalimbali ya maisha yako, kwa kadiri utakavyokuwa ukiendelea katika hali hii ndivyo utakavyo kuwa ukiuona uweza na nguvu za Mungu kwenye maisha yako ukiendelea mstari wa 11 utakuta anasema ‘vaeni siraha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani’ sasa hii inakupa kujua kuwa unatakiwa kupingana na hila za shetani kila siku maishani mwako na hauwezi ukazipinga tu hivi hivi ni mpaka umevaa siraha zote za Mungu, ikiwa ni pamoja na neno la Mungu kujaa kwa wingi ndani yako, kuwa muombaji, na kweli ya Mungu kuwa kwenye maisha yako,



Hii inaweza kuwa moja ya mirango ya adui kwa mtu aliye okoka
Fitina, kule kumfitini mtu au kumsengenya mtu na hauoni shida kufanya hayo, na kule kushindwa kabisa kumtoa mtu moyoni mwako,kushindwa kuachilia,kusamehe, kuendeleza kinyongo, kuacha uchungu uendelee kujaa ndani yako inaweza ikampa ibilisi mrango na ukavamiwa na roho za giza, maana ukiwa kwenye hali hii huna mda wa kuomba, ila unamda wa kulaumu na kunungunika, ikiwa ni pamoja na kujisemea vibaya au kumsemea mwingine.
Kiburi, kule kujaa kiburi na ukaidi, kutokutaka kusikiliza ushauri, kuwaona wengine wote hawana kitu isipokuwa wewe au fulani, na hivyo kutokunyenyekea, wala kushuka kitu ambacho kimesababisha roho za ukengeufu kwa watu wengi leo{uasi} hii imesababisha mirango kwa nguvu za giza.
Tendo la ndoa kabla ya ndoa, au nje ya ndoa kumbuka mtu anapoamua kutoa nguo zake kwa mtu amabaye si mke wake halali, kwa tafsiri ya rohoni anautoa utukufu wa Mungu, au anauvua, hivyo basi anauvua ulinzi, na kwa sababu hiyo Roho za giza zinakuwa na nafasi kubwa ya kuweza kumvaa mtu huyu
Na ndio sababu watoto wa kuhani heli Hofsini na Finehasi walipofanya uzinzi na wanawake waliokuwa wakitumika malangoni pa hema ya kukutania, utukufu wa Mungu uliondoka, na ulinzi wa Bwana ukaondoka na lile sanduku la agano likatekwa, habari hizi utazipata vizuri samweli wa kwanza na kuanzia sura ya pili, kitu nilitaka uone ni jinsi ambavyo utukufu wa Mungu ukiondoka juu ya mtu na ulinzi wa Mungu ukiondoka kwa sababu ya dhambi uwezekano wa mtu kuvamiwa na aroho za giza unakuwa ni mkubwa zaidi.
Kukata tamaa ile hali ya kujikatia tamaa, kuvunjika moyo, kupoteza kabisa matumaini hata kujisemea maneno ya laana, inafungua mirango kwa roho za giza kuvamia maisha yako. Ndio sababu Biblia ikasema Filip 4 :6 msijisumbue kwa neno lolote ; Bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. sasa kule kulaumu kulalamika, kujilaani haja zako zinajulikana na mapepo na sio Mungu. Iyo ndio inayompa adui nafasi kwenye maisha ya watu wengi leo.
MOJA YA MAMBO YALIYO SABABISHA MAELFU YA WATU WA AINA MBALIMBALI KUINGIA KWENYE VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA

Kwa kurithi watoto wengi wanao zaliwa kwenye familia ambazo kuna mambo ya uchawi au wanaabudu mizimu na kufanya mambo ya matambiko huwa wanatolewa kwa pepo au mizimu wangali bado wadogo kadri wanavyoendelea kukua ndivyo wanavyoendelea kuona kama mambo yanayo fanyika ni sahemu halali kwa maisha yao. Nakumbuka safari moja tukiwa kilimanjaro tulifanya huduma na kijana mmoja wa kidato cha pili aliyekuwa amefungwa na nguvu za giza , na tukiwa tunafanya nae maombi alitapika vitu fulani vyeupe vya kushangaza sana. Baada ya kufunguliwa na Bwana Yesu na yale mapepo kumuachia tukapata nafasi ya kukaa nae na kuzungumza nae, alitueleza kuwa yeye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kwenye familia yao na kuwa amekuwa akipelekwa kwenye makaburi na kufanya matambiko na wazazi wake kuanzia akiwa mdogo na akaeleza kuwa alikuwa akilishwa vyakula kama nyama za aina fulani kila alipofika makaburini kwa tambiko, sasa hii ina maana kama Bwana Yesu asinge mfungua angeendelea kuishi maisha ya ushirikina chini ya utawala wa nguvu za giza.namna watoto wanavyoingizwa kwenye vifungowazazi wengi wasio amini huwaingiza watoto wao kwenye vifungo vya ushirikina bila ya wao kujua. watoto wengi wakizaliwa hupelekwa kuchanjwa chale, kwa waganga wa kienyeji au wengine hupelekwa kwa Bibi zao kwa ajili ya mambo fulani ya kimira kama kuzika kitovu, kwa taratibu za kimila, kupewa jina chini ya taratibu za kiganga, z po sara mtoto anaombewa kwa babu zake waliokufa wakati mwingine hizi sara hufanyika makaburini ‘mfano wa sara inayoombwa { mtoto wenu amekuja, mumkumbuke, mumsaidie, tunawakabidhi ni wa kwenu, maneno mengi sana yanatamkwa mara nyngi nkuwa kwa kiluga bila hata ya wao kujua ni nini wanafanya katika ulimwengu wa roho, kumbe katika ulimwengu wa roho yule mtoto anakabidhiwa chini ya falme na mamlaka za giza}Na ndio sababu ukisoma Kumb 18 :10 utakuta anasema Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au Binti yake kati ya moto’ ukiendelea mbele kidogo utakuta anasema ‘wala asionekane mtu aombae wafu sasa u mstari 12a utakuta anasema ‘kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana’Wakati fulani tukiwa na huduma mkoa wa Tanga nilipata nafasi ya kupita mitaani watu wanako ishi asilimia kubwa ya watoto nilio waona walikuwa wamevishwa Hirizi, na vitambaa vyeusi mikononi, shingoni,kwenye miguu wengine walikuwa wamevishwa shanga viunoni, japo hii aina maana mambo haya yako huko tu isipokuwa niliguswa sana nikiwa huko cha kushangaza leo hii hata wakristo wengi wamevalisha watoto wao hivyo vitu, wengine ukiwauliza hata yeye mzazi hajui kwa nini kamvalisha mtoto hicho kitambaa cheusi wengine ukiwauliza atakuambia Bibi yake alimvalisha .
kwa kushiriki mambo ya uchawi na ushirikina wapo wakristo wengi leo hii ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha na mambo ya uchawi na ushirikina bila ya wao kujua mfano kuchangia tambiko, kuhudhuria ibada za wafu, kula nyama za kusongolewa, kunyoa nywele kwa ajili ya aliyekufa, kunywa dawa za kimila, kwenye misiba mingi ambayo watu huamini mambo ya ushirikina huwa wanakunywa Dawa wanafamilia au ukoo mara baada ya mazishi au msiba kuisha . lakini
Biblia imesema wazi kabisa kuwa ‘msishiriki ibada zao’ na ukisoma katika Kumb 14 :1 utakuta anasema ‘msifanye upaa kwa ajili ya aliye kufa.’ Sasa ni muhimu ukafahamu kuwa haya ni moja ya mambo yanayoingiza maelfu ya watu kwenye vifungo
3. wapo waliopata watoto kwa njia za ushirikina
Wapo wanawake ambao baada ya kutafuta watoto kwa mda mrefu bila mafanikio wakaamua kutafuta kwa njia za ushirikina, wengine walilishwa madawa ya kienyeji ili apate mimba, wengine walilazimika kufanya tendo la ndoa na waganga wa kienyeji, wengine walienda kulala juu ya makaburi, na mambo mengine mengi hakuna hata muda wa kutosha kuelezea kila kitu, kitu nataka ufahamu ni hiki kuwa huyo mtoto aliyepatikana kwa namna ya uchawi na ushirikina ni lazima tu awe chini ya utawala wa Nguvu za giza {kwenye vifungo} {maana agano la kupatikana kwake lilifanyioka wakati wa kutungwa mimba} yaani mimba ilipokuwa inatafutwa. Na mara zote mtoto wa namna hii kuwa na tabia za tofauti huwa na uwezo wa kuona vitu vya tofauti, maana roho za giza zina hati miliki juu yake,
4. Kukubari huduma za kishirikina
Wapo watu ambao walipoibiwa tu wakashauliwa kwenda kuagua kitu ambacho ni chukizo mbele za Bwana Kumb 18:10b ‘Wala asionekane mtu atazamae bao,,,,’ ukiendelea mbele kidogo utakuta
anasema ‘wala mwenye kubashiri, wala mshihiri, Wala mtu alogae kwa kupiga ufundo shida ni hii kuwa wapo wakristo wengi sana leo wanao muhuzunisha Bwana kwa kushiriki au kukubariana na huduma za kishirikina na wakati huo huo wanamuabudu Mungu, wakristo wengi leo wamependa mambo ya Unajimu kwa mfano Unajimu wa Nyota, matumizi ya vitu mbalimbali kama karata, kubashiria bahati kupiga ramli, kutegua tego,
5. kuzindika nyumba
Wapo watu wengi leo walio danganywa kuwa kuna kuweka ulinzi kwenye nyumba zao Hivyo wakaruhusu waganga kuja kuchimbia vitu Fulani kwenye Nyumba zao na matokeo yake huwa inakuwa ni kupuputika kwa familia ikiwa ni pamoja na kukaribisha magonjwa na mikosi kwenye familia, ikiwa ni pamoja na vilio visivyoisha, maana mnaikabidhi ardi yenu chini ya utawala wa nguvu za giza, sasa kwenye kitabu changu cha kwanza kijulikanacho kama {PAMBAMBANA DHIDI YA NGUVU ZA GIZA}nilipokuwa natoa utangulizi wa masomo haya nilitoa ushuhuda jinsi tulivyo fanya huduma ya kufukua mazindiko kwenye familia Fulani maana familia iligeuka maali pa maombolezo, mtoto wa kwanza na wa pili walikufa katika hali ya kutatanisha mtoto wa tatu akawa yuko taabani, ukimtazama mama yake hajiwezi kwa ugonjwa ndipo mzee mwenye nyumba akakumbuka agano la ardi yake na mapepo, nakumbuka
Tulipomaliza kufukua mahali palipo chimbiwa tulikuta vitu vya ajabu kweli,lakini ninachotaka ujue ni kuwa mara baada ya kufukua vitu vilivyo chimbiwa zaidi ya miaka kumi iliyopita tulivichoma moto, na familia yote wakaamua kumpa Bwana maisha kuanzia pale, yule mgonjwa waliyekuwa wakitegemea angekufa mda wowote na kukamilisha idadi ya watoto watatu kufa maana alikuwa mahututi, alipokea uzima toka kwa Bwana Yesu, mpaka leo hii nikienda kwenye ule mkoa namkuta akiimba kwaya ya vijana kanisani kwao. mateso na vilio vikaondoka.kitu nilitamani uone ni hiki kuwa Bwana asipoulinda mji yeye alindae akesha bure,
USICHANGANYE NGUVU ZA MUNGU NA SHETANI NI HATARI
acha kumchanganya Mungu kabisa, maana utakufa. ukiamua kumtegemea Bwana Yesu, mtegemee yeye kwa asilimia mia moja na si vinginevyo maana wapo wanaopenda kuchanganya nguvu za Mungu na za Ibilisi kumbuka hilo ni kosa kubwa na Nyuma yake kuna laana na mauti utaishia kufa kifo kibaya na aibu yako itajulikana..maana ukisoma Kumbukumbu la torati 28:4 -13 utaona Mungu akitoa Baraka ikiwa watu watamtegemea na kumuamini yeye peke yake, anaanza na kuzungumza habari za uzao wa tombo lako utakavyobarikiwa, anazungunza habari za adui zako kupigwa na kuanguka mbele yako, na jinsi ambavyo kila utakalo lifanya litabarikiwa, ameeleza mambo mengi sana ambayo anatamani yafanyike Baraka kwenye maisha yako, endapo utatii na kufuata maagizo yake, Lakini ukisoma ule mstari wa 14 anasema "msipogeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lolote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia." Sasa lile neno msipogeuka kwa tafsiri nyingine msiponiacha na kufuata mambo ya ushirikina{miungu mingine} maana ni rahisi sana kudanganywa kuwa uko msaada kwenye uchawi, na mambo ya ushirikina lakini nataka ujue wazi leo hii kuwa, huko ni kijitafutia laana na mauti yako mwenyewe. Maana hakuna kitu Mungu anapingana nacho kama sisi kumchanganya yeye na miungu mingine.
Na ndio sababu ukisoma ule mtari wa 15 anasema ‘lakini itakuwa usipotaka kuisikiliza ile sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata’. Ukiendelea mbele kidogo anaelezea hizo laana mstari wa 16 utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. litalaaniwa kapu lako na chombo cha kukandia {kapu lako : {kwa tafsiri nyingine utalaaniwa uchumi wako}anaendelea ‘BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa katika yote utakayotia mkono wako kufanya, hata uangamie na kupotea upesi’ {kumbuka sio mapepo, ila Bwana atafanya } na ndio sababu kuna wakati shida yako inaweza ikaombewa na kila mtumishi na isipatiwe ufumbuzi isipokuwa ni mpaka Mungu atakapokuja kumpa mtumishi mwingine neno la maarifa juu ya dhambi yako na kwamba uondoke kwenye maagano ya ushirikina uliko ndipo uvumbuzi wa shida yako utakapotokea, na ndio sababu ni bora uwe na uadui na shetani Mungu atakusaidia, kuliko ukawa na uadui na Mungu hii ni hatari kubwa maana hatakuwepo wa kukusaidia.
Ukisoma ule mstsri wa 28 anasema ‘BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu na kwa bumbuazi la moyoni utakwenda kwa kupapasa papasa mchana,kama apapasavyo kipofu gizani wala hufanikiwi katika njia zako ; nawe siku zote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.’ Sasa ukiendelea mbele kidogo utaona jinsi ambavyo utachumbia mke na mtu mwingine atalala nae {watamchukuwa} na mambo mengine mengi ambayo yatakupata tu kwa sababu umeabudu miungu mingine. Na kama hayo mambo hayajakupata wewe hata ikiwa yamekupata kwa sehemu, basi uwe na uhakika watoto wako watarithi mateso ya dhambi yako. Maana Mungu hupatiliza maovu, alihaidi kupatiliza maovu ya Baba kwa mwana, ukisoma { Kutoka 20 :4 anasema ‘usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu kilicho juu mbinguni, wala kilicho majini chini ya Dunia ; Usivisujudie wala kuvitumikia kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu ; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,’
Sasa Mungu ameshasema kuwa wana watapatilizwa maovu ya Baba zao tu kwa sababu Baba zao waliabudu miungu mingine. Ili kuepuka mambo haya yote usimchanganye Mungu maana kuna watu leo wanaenda makanisani na bado wanairizi, bado wanashiriki mambo ya giza, bado wanashiriki mambo ya jadi na mila, hivyo basi ni muhimu sana ukawa na maamuzi ya kumtumikia Mungu peke yake na si vinginevyo

Mambo yanayotokea nyumba inapokuwa imezindikwa
Nyumba ikizikilicndikwa maana yake imekabidhiwa kwa pepo kwa tafsiri nyingine watoto wanakuwa wamekabidhiwa pia maana ni sehemu ya familia, miradi inakuwa imekabidhiwa pia biashara, ndoa, pamoja na kazi, hii ni hatari sana, na watu wengi sana wanaoishi kwenye Nyumba za kupanga zilizozindikwa huwa wanapata shida sana ya mapambano na roho za giza mara kwa mara wachache huwa wanapewa macho ya rohoni kujua kuwa ziko falme mbili zinapambana mahali hapo.Biblia inaposema katika {Yoshua 1:3 } kila mahali zitakapo kanyaga nyayo za miguu yenu nimewapa,
haina maana ufike tu hotelini au nyumba ya wageni na kulala tu, au uamie tu kwenye Nyumba na kuanza kuishi bila kufanya chochote au uinmgie kwenye basi na kustare kama abiria wengine hiyo naifananisha na imani pasipo matendo maana kwa tafsiri halisi wewe mtoto wa Mungu kupewa kila mahali nyayo za miguu yako zinapokanyaga ni kupateka mahali hapo na kuvuinja falme zingine zilizokuwa zinatawala na kuupanda ufalme wa Mungu na ndio sababu Mungu alimwambia Yeremia kitu alichotakiwa kufanya ukisoma Yeremia 1:10 anasema ‘Angalia nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme’ kwa tafsiri nyingine nimekupa mataifa nimekupa na falme utawale ukiendelea pale mbele utakuta anasema ili….. sasa neno ili linatafsiliwa kama sababu, sasa ni sababu ipi ya M ungu kumuweka Yeremia juu ya mataifa na juu ya falme utakuta Mungu alikuwa na lengo la kungoa, na kubomoa, na kuharibu kazi za ibilisi alafu aujenge na kuupanda ufalme wa kwake. Hivyo basi mambo haya ambayo mungu aliyatarajia yalitegemea sana uelewa wa Yeremia kwa habari ya yeye kuwekwa juu ya mataifa na juu ya falme.

6. matumizi ya hirizi na baadhi ya vifaa vya ushirikina
Maelfu ya watu leo wameingia kwenye vifungo kwa sababu walikubari kupokea hirizi na wengi wao wanazitumia kwa siri wakifikili kuna ulinzi na usalama kumbe ni kujiingiza kwenye mikataba ya nguvu za giza,wako wengine ambao wameziweka kwenye Magari yao, wengine kwenye vitanda vyao, wengine wameshonea kwenye nguo zao, ilimradi tuu isionekane, ni muhimu kufahamu kuwa Mungu wetu yu kinyume cha Irizi ukisoma Ezekiel 13:20 anasema ‘ Basi Bwana Mungu asema hivi mimi ni kinyume cha Irizi zenu…….’ Sasa ukianzia pale mwanzo kidogo utakuta anatoa ole, kwa wanawake wanao shona irizi.. na utaona jinsi ambavyo matumizi ya irizi ni kwa ajiri ya kuondoa Roho za watu kishirikina. Na ndio sababu Biblia ikasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Maana yake ni kuwa hawana ufahamu,juu ya mambo wanayoyafanya na ndio sababu maelfu ya watu wameingia au wameingizwa kwenye vifungo vya ibilisi wakidhani wanatafuta ulinzi,usalama,amani,furaha,maisha mema, na matokeo yake kuwa vilio na majuto.

Je kuhusu shanga bangili na mikufu

Ni kweli kabisa kuwa wapo watu wengi leo wanaopenda kutumia vitu vya ulembo kama Shanga, maana zipo zinazotengenezwa kwa mfumo wa kuvaa hata wanaume pia, mfano ni zile za mikononi, na wapo wanawake wanaopenda kuvaa zile za kiunoni, mikufu, bangiri, pete, mapambo ya ndani kama vinyago na vibuyu, ni muhimu sana kuwa makini hapa maana kwenye ulimwengu huu wa utandawazi kila kitu huonekana kuwa ni cha muhimu na chenye thamani kwa Binadam.
Ni katika ulimwengu huu tunaoishi tunapotakiwa kuwa makini sana na kila chaguo la jambo tunalotaka kufanya kama wacha Mungu, na si tu kufanya kwa sababu wengine wamefanya, tunahitaji kuwa na macho ya rohoni hasa tunapofanya maamuzi ya maisha na mambo ambayo tungetamani yaambatane na maisha yetu, kuna kitu kiaitwa macho ya rohoni tunahitaji kuwa na macho ya rohoni ili kuepukana na vitu amabavyo miili yetu inaweza ikavutiwa navyo pasipo ufahamu wa mambo ya rohoni ikawa ndio tunapelekwa kwenye vifungo

Biblia inaposema katika {Kor 3 :15} kuwa ‘na amani ya kristo iamue mioyoni mwenu….’ Maana yake ni hii kuwa anayeleta amani ya kristo mioyoni mwetu ni roho mtakatifu peke yake , sasa kwa nini akasema amani inayotakiwa iamue mioyoni mwenu ni ya kristo hii ina maana zipo amani nyingine zinazoweza zikaamua moyoni mwako na matokeo yake zikasababisha mambo magumu sana kwenye maisha yako, ikiwa ni pamoja na milango kwa adui,
Sasa ni muhimu kutambua kuwa ni wajibu wa Roho mtakatifu kuamua kwa niaba yetu, kwani ndie kiongozi wetu, msaidizi na mwalimu wetu. lakini asipopewa nafasi kwenye maisha yetu hukaa pembeni akihuzunika kwani hawezi kukulazimisha kufanya jambo, ‘Efeso 4:30 wala msimuhuzunishe yule Roho mtakatifu wa Mungu,ambaye kwa yeye mlitiwa mihuri hata siku ya ukombozi’ na sehemu nyingine ya Biblia inaonyesha jinsi ambavyo Roho hututamani kiasi cha kuona wivu yaani huwa anatamani kama angeamua kwa niaba yetu, angefanya kila kitu kwa niaba yetu, sasa kwa sababu maisha yetu hayana nafasi ya Roho mtakatifu kufanya kwa niaba yetu ndio sababu tunashindwa kuyafahamu mambo ya rohoni, na mipango ya Adui iliyo katika siri kubwa kuharibu maisha Yetu. na ndio sababu pia ukisoma Rumi 8 :26a anasema ‘kadharika Roho nae hutusaidia udhaifu wetu, miili yetu ina madhaifu mengi sana, mfano tamaa, tunatamani kila kitu hata bila kujiuliza maswali wakati mwingine, wala kutafuta maana ya hicho kitu ni nini, hata kuna baadhi ya vitu tumejiingiza kwavyo tu kwa sababu labda ukifanya ndio unaonekana wa kisasa zaidi, sio vibaya kuonekana wa kisasa isipokuwa swali la kujiuliza ni je ninaliolifanya au ninalotaka kulifanya linampa Mungu utukufu ? na je Adui hawezi akapata nafasi kwa njia hii ? korosai 3 :17 ‘Na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu’ maana yake ni hii kila unalolitamka kinywani mwako au muonekano wako au unalolitenda, limtangaze kristo, limdhihilishe kristo, limfanye kristo apate utukufu. Kitu ambacho si rahisi kama Roho mtakatifu ajapata nafasi ya kwanza kwenye maisha yako,
Sasa ukiunganisha na mapungufu tuliyo nayo inampa ibilisi milango ya uvamizi kwenye maisha
yetu
Yapo mambo mengi ambayo kwa hayo tunakuwa tumejiingiza kwenye vifungo bila ya sisi kujua ukielewa kitu cha namna hii hautaacha kumpa Roho mtakatifu nafasi ya kwanza katika kuamua mambo yako na kuhakikisha kuwa inayoamua ndani yako ni amani ya kristo.
mambo mengine yanayokupa ulazima wa kuhakikisha anayeamua moyoni mwako ni ni Roho mtakatifu
kujua fikra za ibilisi 2korinto 2 :11 ‘shetani asije akapata kutushinda kwa maana hatukosi kuzijua fikra zake’ fikra zake ni mipango yake ya uharibifu juu ya maisha yako sasa ili asikushinde ni lazima uzijue kwanza fikra zake, mbinu zake za uharibifu,na jinsi anavyotaka kukuingiza kwenye vifungo upo msemo wa kiswahili usemao { kumjua adui ni nusu ya kumshinda} sasa basi ile tu kujua kuwa kwa kufanya hili nitakuwa nimempa ibilisi nafasi na hivyo kutokufanya ni kumshida Adui teyariUshuhudanikiwa nafanya huduma hii ya kufunguliwa katika mkoa fulani yupo binti ambae alikuwa amepagawa na Roho za giza, sasa Baada ya kufunguliwa na bwana yesu nilipata nafasi ya kuzungumza naye na kutaka kujua iyo shida ilianzaje, alieleza kuwa siku moja ya jumamosi alipewa rifti na watu asiowajua lakini walidai kuelekea alikokuwa akielekea yeye,Anasema akiwa kwenye gari alipewa Biskuti na hakuona haja ya kukataa, kwa sababu ilikuwa ni biskuti tu, anasema walipo mshusha tu alipotakiwa kushuka gafra akasikia kutapika na alipotapika zilikuwa ni nywele za binadamu, alic`hanganyikiwa hakuelewa nini. Na kuanzia hapoalianza kujisikia vibaya mwilini na vitu vya ajabua vikaanza kutokea kwenye maisha yake,Anasema kuna wakati akawa anajikuta anatamani tu kukaa uchi, bila nguo watu wote wakiondoka ndania anafunga milango yote anavua nguo zote, alinieleza mambo mengi sana ya ajabu, kitu nilitaka uone ni hiki kuwa milango ya adui ilikuwa ni kwenye ile Taxi na zile biskuti, sasa sisemi usipande taxi wala usipokee vitu isipokuwa Roho mtakatiifu aamue kwa niaba yako,Shida ni hii kuwa kama Roho wa Mungu hachukui nafasi ya kwanza kwenye maisha yako hutaweza kabisa kuzijua fikra za Ibilisi kwenye maisha yako na hatimae kujikuta uko katikati ya vifungo vya adui.
Miitego ya ibilisiZab 91 :3 ‘Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji na katika tauni iharibuyo’ ndugu unayefuatilia mafundisho haya ni muhimu ukatambua kuwa kuna mitego mingi sana ya ibilisi kila siku kwenye maisha yetu, mitego ambayo unatakiwa kuitegua kwa neno la Mungu ,maombi na kwa kuongozwa na Roho mtakatifu katika kila unalolifanya.na ndio sababu Biblia ikasema msimpe ibilisi nafasi maana yake ni kuwa jambo lolote utalolifanya bila msaada wa Roho mtakatifu linaweza likampa ibilisi mlango wa kukuingiza kwenye vifungo maana anatutafuta usiku na mchana Biblia inaonyesha wazi kabisa kuwa anawashitaki wateule wa Mungu mchana na usiku, na pia ni kama Simba aungurumae anawatafuta wateule awameze, Hebu fikiria kama katika kila masaa 24 kwenye kila sekunde inayopita kuna mtego wa ibilisi unakutafuta, wewe unajipangaje au umejipangaje.Na mitego yote ya ibilisi ina lengo la kuwaingiza watu kwenye vifungo vya nguvu za giza na kuwabana mahali ambapo watendelea kunyanyasika,.na hii ndio sababu unatakiwa kujifunza kuwa mtu wa rohoni maana Roho wa Bwana atakuongoza katika kila unalolifanya, na kukuepusha na mitego ya ibilisi.na kukupa macho ya rohoni kujua nini upokee na nini usipokee, nini ufanye na nini usifanye, wapi uende wapi usiende, je kuna ulazima wa kushiriki hayo mazungumzo au hakuna ulazima, je ununue iyo bidhaa ya mamna iyo au usinunue, je ununue leo au kesho, je uupokee huo ushauri au usiupokee, je uvae iyo nguo kwenye hicho kikao au uvae nyingine, hii itakusaidia sana kutoishi maisha ya kawaida na kuepukana na mitego ya ibilisi.Na ndio sababu Biblia ikasema katika 1korinto 2 :15 ‘Lakini mtu wa Rohoni huyatambua yote, wala yeye atambuliwi na mtu’ mtu wa rohoni ni nani ni Yule aliyempokea Bwana Yesu na anayeongozwa na Roho mtakatifu, hivyo roho mtakatifu kumpa nafasi ya kujua mambo mbalimabali yanayoendelea katika ulimwengu wa Roho, Amosi 3:7 Hakika bwana hatafanya neno lolote bila kuwafunulia watumishi wake, manabii siri zake, hii ina maana Mungu kuna vitu hata ruhusu kwako mpaka amekujulisha na Mungu anapokujulisha kama icho kitu ni kibaya maana yake anataka ukipinge, au ukikatae, au ukiepuke, hivyo basi kama kuna mtego wa ibilisi mbele yako au mkakati wa adui, wa kukuingiza kwenye dhambi, au vifungo, Mungu anakuapa kujua. Na unapewa kuyafahamu Mambo ambayo wengine hawayajui wala hawawezi kuyatambua na ndio sababu Biblia ikasema mtu wa rohoni huyatambua yote, kwa vipi ? kwa msada wa Roho mtakatifu {ni muhimu kuelewa kuwa hatuwezi kuyajua mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa Roho mpaka tumekuwa katika Roho}
Ukisoma Daniel 2 ;18 anasema ‘Ndipo Danieli akafunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamuhimidi Mungu wa mbinguni’
Sasa ukianza nyuma kidogo na hii habari utagundua ilikuwa ni shida iliyompata Mfalme nebukadreza, na vile ambavyo hakuna mtu mwingine angeliweza kujua jambo lolote isipokuwa ni yule tu wa rohoni, kwa sababu Danieli alikuwa ni mtu wa rohoni Bwana alisema nae rohoni jambo ambalo wenye hekima, na wachawi wote walishindwa kuliletea uvumbuzi, lakini kijana mmoja wa Rohoni aitae Danieli, akawa ana jibu na kusababisha amani kwa nchi nzima.
Ndugu msomaji isikutishe hii kuitwa mtu wa Rohoni au la, Biblia imesema wazi kabisa ‘Rumi 8 :14 kwa kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu’ hivyo basi kama umeokoka Roho mtakatifu yuko ndani yako, maana huwa anashuka kwa ajili ya kuwaongoza maelfu ya watu wanaoingia kwenye orodha ya kuitwa wana wa Mungu, maana ndie anayetakiwa kumfundisha na kumuongoza kila anae ingia katika maisha mapya sasa shida ni kuwa watu wengi huwa tuna muhuzunisha, na wakati mwingine tunamzimisha kabisa.

Ingekuwa kama tungejua jinsi tunavyotafutwa na ibilisi usiku na mchana na hatuwezi kuona kwa sababu tunaishi mwilini na kuwa Roho mtakatifu anatakiwa kuona kwa niaba yetu kama ni balaa atuepushe, kama ni mauti atuepushe,na kuwa kama kuna jambo lolote atuajulishe kitu cha kufanya. Tungeyatambua hayo tungeudumisha uhusiano wetu na Roho mtakatifu.
maana kadri utavyoendelea kuudumisha uhusiano wako na Roho mtakatifu kwa maombi, na kwa kulisoma neno, ikiwa ni pamoja na akujiepusha na uovu unampa roho mtakatifu nafasi ya kuyafungua macho yako ya Rohoni,na masikio yako ya Rohoni hivyo basi ukianza kusikia na kuona Rohoni hakuna namna adui anaweza akakupata,
Maana kuna wakati mwingine utaambiwa usipande iyo Gari, au usichukue iyo nguo. Au usitumie iyo zawadi, au usinunue icho kinyago, au usinunue huo mdoli, au usile icho chakula,


Nakumbuka tukiwa tunafanya huduma ya ukombozi mahali fulani Dada mmoja alikuwa amevamiwa na nguvu za giza tu kwa sababu alilithi gauni la shangazi yake kumbe baada ya shangazi mtu kufariki Roho za giza zikabaki kwenye Nguo zake tulipokuwa tukiamuru zile roho za giza zimtoke zilipiga kelele na kusema tunataka gauni letu la marehemu, amechukuwa gauni letu, kwa kweli sikuelewa sana, isipokuwa mara baada ya kumaliza ile huduma nilipata nafasi ya kuzungumza nae na kumuuliza endapo kuna kitu chochote amekirithi ni cha marehemu ndipo aliponijulisha kuwa ni kweli kuna gauni la Shangazi alipokufa nikalichukuwa huwa ninalivaa ila kuanzia nilipoanza kulivaa kuna vitu niliona vimebadilika sana mwilini mwangu.
Kitu ninachotaka uwe mwangalifu ni hiki kuwa kuna wakati utatakiwa kuombea hata nguo kabla ya kuivaa, lakini anayetakiwa kukumbusha na kukuambia kama uombee au la, si mwingine isipokuwa ni roho mtakatifu. Na ndio sababu ukisoma katika Zekaria 3 :4 anasema ‘Nae huyo akajibu akawaambia wale waliosimama mbele yake akisema mvueni nguo hizi zenye uchafu, kisha akamwambia yeye tazama nimekuondolea uovu wako nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi,,,,,,,,’ kitu nilitaka uone ni jinsi amabavyo unaweza ukabeba matatizo,uovu,uchafu, shida tu kwa sababu ya mavazi, na ndio maana baada ya huyu ndugu kutolewa yale mavazi yake machafu uovu wake uliondolewa hii ina maana uovu ulikuwa kwenye mavazi. Na kumbuka ndugu mmoja aliniuliza swali sasa utajuaje hili vazi lina nguvu za giza na hili halina,
Ndugu msomaji ndio maana tunasisitiza uhusiano wa mtu binafsi na Roho mtakatifu maana si kweli kwamba mavazi yote yana mapepo isipokuwa kunawakati utakutana na mtego wa namna hiyo na kama hautakuwa na macho ya rohoni itakuwa rahisi sana kwa wewe kutekwa na ibilisi.
7/ kuhuzuria au kuishi maeneo yenye utawala wa kipepo
Ndugu msomaji wapo watu ambao huchukulia mambo haya kirahisi wapo watu amabao hupenda kuhuzuria maeneo ya matambiko hata kama wao wameokoka, wengine hawaoni shida huhudhuria vikao vya sadaka kwa miungu wengine huudhuria siku ambapo zile nyama zinaliwa ambabazo ni batili, wengine hudiliki hata kunywa zile dawa ambazo wao jadi na mila, wanaziita kinga ya ukoo, wengine huwa wanadai wanawasindikiza wengine kumbuka kadri unavyoendelea kuhudhuria kwenye hayo maeneo ndivyo unavyoendelea kufungua mirango kwa Adui hutajua ni saa ngapi mapepo yalikuvaa, maana ulinzi wa Mungu huondoka na kwa sababu yeye ni Mungu mwenye wivu ukijiingiza kwenye miungu mingine ulinzi wke unakuacha na laana yake inaambatana nawe, na Biblia inaonya , Kumbu 4 : 23 jihadhalini nafsi zenu msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu alilofanya nanyi mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu chochote, ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto ulao Mungu mwenye wivu.’ Sasa ukiufuatilia huu mstari utakuta anasema jihadhalini nafsi zenu. Msije mkaanza kuabudu miungu maana washirikina wengi leo hawajui ni lini walianza kuamini hivyo vitu wanavyo amini pia hofu ya Mungu imewatoka na ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa hiki ndicho kilichozaa huu mstari bandia wa biblia {jisaidie nami nitakusaidia} watu kutaka kuhalalisha kumchanganya Mungu na shetani,kuchanganya mambo ya ushirikina na Mungu. {hatari} kumbuka Mungu ni moto ulao na ni mwenye wivu.





8/ wengine majina yao yamewaingiza kwenye vifungo
Ndugu msomaji wa mafundisho haya ukifuatilia leo majina mengi sana amabayo watu wanayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakiendana na maisha yao, sababu ni hii kuwa jina lina sehemu kwenye maisha ya mtu, ukifuatilia malaika Gablieli wakati anamwambia Yusufu sababu za kumuita mtoto jina Yesu utagundua kuwa aliitwa Yesu kwa sababu ndie aliyekuja kuwaokoa wanadamu na dhambi zao kwa iyo jina Yesu ndani yake kulikuwa na ukombozi wa dhambi za watu, hebu soma
"basi alipokuwa akisafiri tazama malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto akisema ‘Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu MAANA YEYE NDIE atakaye waokoa watu wake na dhambi zao." Sasa lile neno maana tunaweza tuka sema kwa sababu, fikilia kama Yusufu angeamua kumuuliza malaika kwa nini mtoto aitwe Yesu? Na tusimuite jina jingine, Malaika angemjibu kwa sababu ndie atakayewaokoa watu na dhambi zao. Hivyo unaweza ukaona kuwa ndani ya jina la Yesu kulikuwa na ukombozi, na ndio maana leo tukilitaja kuna mambo ya tofauti yanatokea, pia zipo sababu nyingi zinazowafanya watu waape watoto majina wanayo wapa
Yapo majina kama Taabu, Shida, Majuto, kibaya, Cha usiku, Mbutolwe hili ni la kilugha maana yake kwenye matatizo, yapo mengi yanayofanana na haya sasa sisemi majina kama haya ni mabaya isipokuwa natamani wewe unaye muamini Mungu upate uwanja mapana wa maarifa, maana asilimia kubwa ya watu waliopewa majina haya majina yao yanaendana na maisha yao, maana Jina linanafasi kwenye maisha ya mtu. Hivyo basi jina linaweza likafungua mlango kwa roho za giza kumiliki maisha ya mtu. Hebu tuangalie mfano mwingine ukisoma Mwanzo 35:16-18 anasema "wakasafiri kutoka betheli hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrasi Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa na utungu wake ulikuwa mzito ikawa alipokuwa anashikwa na utungu mzalisha akamwambia usiogope maana sasa utamzaa mwanamume mwingine ikawa hapo katika kutoa Roho yake maana alikufa akamwita jina lake Beloni lakini lakini Baba yake akamwita benjamini" sasa unaweza ukaona mazingira jina lilivyo tolewa, jina lilitolewa mama akiwa anakufa na unaweza ukajiuliza swali kwa nini Yakobo alipofika akambadilisha mtoto jina? Jina a la kwanza halikutolewa kwenye mazingira ya baraka isipokuwa mazingira magumu yaliyojaa uchungu. Lakini pamoja na hayo yapo majina ambayowatoto walipewa na waganga wa kienyeji, watu wa mira, wazee wa jadi, majina mengine yalitolewa kwenye matambiko ibada za kuwaombea watoto kwa wafu majina haya huambatana moja kwa moja na roho za giza.
Jifunze kutangua maneno mabaya ya watu kwenye maisha yako. Mtu anapokuambia utakufa palepale mwambie sifu, utafeli sifeli, jifunze kutangua laana za maneno kila wakati maana maneno ya mshirikina au mchawi yanaenda kutengeneza kitu katiaka ulimwengu wa roho ambacho uanaweza ukakitangua hapohapo anapokisema.
NINI HUTOKEA KWA MTU ANAPOKWENDA KWA MGANGA WA KIENYEJI
------ Huingia kwenye laana ya kuabudu miungu mingine na kuitegemea, maana mganga wa kienyeji hutumia mizimu kutatua matatizo yake, hivyo basi mtu huyu pia anakuwa amejiingiza kwa hiari kwenye utawara wa nguvu za giza.
------mtu anapochanjwa chale kinachokuwa kinatafutwa ni Damu, kwa ajili ya kufanikisha agano Fulani na mapepo, kwa hiyo Damu inapotolewa kwa kuchanjwa wakati mwingine mganga huwa akisema maneno ambayo mtu anakuwa hajui maana yake, hivyo unapochanjwa chare unaingia kwenye mkataba wa mwili wako na mapepo, unaubinafsisha mwili kwa roho za giza. Kwamba roho za giza ziwe na maamuzi juu ya mwili wako.
------umewahi kujiuliza kwa nini mganga wa kienyeji hutoa masharti amabayo mtu asipofuata anakuwa katika hali ya Hatari, sababu ni hii, ili aendelee kuzitimizia roho za giza matakwa yao kupitia huyu mtu maana huyu mtu anakuwa umefanyika sehemu ya utendaji katika ofisi za kipepo.
-----roho za ushirikina zinamvaaa, imani yake inaamia kwenye roho za giza, kunaanza kutegenezeka urafiki kati ya mtu huyu na roho za giza hivyo basi kila gumu atakalo kutana nalo, utatuzi wa kunza utakuwa ni mganga wa kienyeji na mambo ya ushirikina, maana ufahamu mtu unakuwa umetekwa, mwenye vifungo, watu wanamshangaa lakini lakini yeye anajiona yuko huru,yuko sahii.
-----Irizi anayopewa mtu kwa mganga ni ishara ya kukubaliana na kubeba mizigo ya mapepo kwenye maisha yake ikiwa ni pamoja na Roho za mauti, na ukitaka kujua irizi ni mbaya watu huwa wanaificha. Na kila wakati ni nyeusi, Mungu amekataa matumizi ya Irizi, Ezekieli 13:18 anasema "useme hivi,Ole wao wanawake wale,washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono"……ukiendelea mtari wa 20 anasema "Basi Bwana Mungu asema hivi, tazama mimi ni kinyume cha Irizi zenu….."
MATOKEO YA WATU KUSHIRIKI MAMBO YA USHIRIKINA.
Unaambukizwa rohoo za ushirikina.
Anaambukizwa roho za ushirikina kwa njia ya uvuvio wa kipepo, Ghafla anaanza kupenda na kuzoea mambo ya kichawi,anaanza kujitoa kwa shetani na kuwa teyari kumuabudu, unaanza kuwa muadilifu katika kutimiza yanayohitajika kama kutoa sadaka ya damu, na mambo mengine ya aibu. Nimefanya counseling {ushauri} na mabinti ambao wazazi wao waliwataka kufanya nao tendo la ndoa wengine wameshafanya tendo la ndoa na wazazi wao kwa siri nikagundua. sababu kubwa ni roho ya ushirikina ndani ya mzazi. Maana pia wako wazazi ambao hawapeleki mtoto shule mpaka wameenda kwa waganga wa kienyeji kwanza.
Sasa kitu shetani anakifanya ni kuhakikisha washirikina wamekuwepo kila mahali ili kulahisisha utendaji wake wa kazi, na moja ya kazi kubwa ya washirikina ni kuambukiza imani ya kishetani kwa watu wengine. Na ndio sababu unatakiwa kuwa muangalifu maana si wengi waliozaliwa na Roho za uchawi, wengingi wamevuviwa na pepo kwa kushiriki mambo Fulani Fulani.
Mara nyingi Mambo haya huambatana na washirikina
{a}Roho za mauti, mtu huyu anakuwa katika hali ya kufuatiliwa na Roho za mauti, wengi wao hufa vifo vya gafra, Ajari zenye utata,
{ b} Kufungwa kizazi, wapo watu ambao waliwahi kushiriki mambo ya ushirikina na wamekuwa tasa hawawezi kabisa kupata watoto mpaka yale mapepo yaliyoshikilia kizazi yatakapoachia icho kizazi.japo haina maana kila Tasa ni roho za Giza. Ikiwa uliwahi kushiriki mambo ya ushirikina na unashuhudiwa moyoni kuwa Roho za mauti zinakufuatilia Muamini yesu leo akufungue maana yeye ni mkuu kuliko hizo Roho za giza ukisoma Ebra 2:14 anasema "basi kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo ili kwa njia ya mauti amuharibu
yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa"
{ c } kutofanikiwa watu wengi waliowahi kushiriki mambo ya kishirikina nyuma yao huwa kunakuwa na hali ya kutokufanikiwa kuna hali ya kuharibika kwa mambo anaweza akawa alinunua gari gafra inapata ajali, alikuwa na Duka linaungua, mara anaporwa mali yote, mara anafukuzwa kazi, ili mradi tu aishi maisha ya kuchanganyikiwa sababu huwa inakuwa nyuma ya mafanikio ziko roho za giza.
{d} Roho za kukataliwa watu wengi leo wanaofuatiliwa na nguvu za giza kwa sababu walishiriki mambo ya ushirikina huwa nyuma yao kunakuwa na kukataliwa, hali ya kuchukiwa, hata ukipendeza hakuna mtu anakuambia umependeza, hata ukiwa na mawazo mazuri hakuna anaye yataka mawazo yako, kwa wakaka hata ukiwa na kila kitu hakuna Dada anayetamani kuolewa na wewe, kwa akina dada hata kama kuna kaka alisha kuchumbia anakuja kukuacha gafra na hataki tena kukuoa, kwa wafanyakazi inawezekana ofisini mtu ni mchapa kazi lakini hakuna mtu anajali hata kuna wakati mtu huyu huwa anajisikia vibaya.sehemu kubwa ya mambo haya huwa inakuwa ni Roho za kukataliwa.na mambo mengine mengi ambayo yanafanana na haya
Hivyo basi ikiwa unakabiliana na hali za namna hii uwe na hakika siyo mapenzi ya Mungu japokuwa yapo mambo mengine ya kawaida kabisa yanayoweza yakasababisha mtu akaonekana amekataliwa, mfano kutokujijari {usafi} hasa mabinti, kutokuwa mtii, kutokuwa mnynyekevu, kutokokujizuia,kutokujikubali,kutokujiamini, na maengine mengi yanayofanana na haya
Unavyoweza ukayatambua moja ya matendo ya Uchawi na Ushirikina
Ibada za wafu, kuagua, kuzindika, kuongea na wafu, Ibada za mapepo,unajimu wa nyota,sadaka ya damu, Ngoma za matambiko, kuamini waganga wa kienyeji, uwezo wa kuona mambo yasiyoonekana, na kujua mambo kabla hayajatokea, pasipo Nguvu ya Yesu, uwezo wa kusafiri mbali nje ya mwili wako, wengine huona kama anapaa hewani, utumiaji wa vifaa vyovyote vya kichawi, kushiriki ibada za kimila, hivyo kuna umuhimu wa kuwa muangalifu sana kama kuna baadhi ya haya mambo umekuwa ukihusika nayo.
LAANA
Ukisoma kamusi ya Kiswahili ijulikananyo kama ‘oxford kamusi ya kiwahili sanifu’ utakuta wameelezea neno Laana kuwa ni ukosefu wa radhi za mwenyezi Mungu; hasira ya Mungu. Au apizo atoalo mtu kwa mtu mwingine ili afikwe na ubaya, uovu,msiba, au hasira ya Mungu.
LAANI neno laani limetafsiliwa kama, shtakia kwa Mungu, au ombea uovu.
Ndugu msomaji yapo mambo mengi sana amabayo yanaweza yakasababisha hasira ya Mungu kwa mtu , na kusababisha mtu ashindwe kabisa kupokea Baraka kutoka kwa Mungu. Kwenye maisha yake.
Hivyo basi hasira ya Mungu {laana} inaweza ikampata mtu yeyote ambae atahusika na haya yafuatayo.
{a} Laana ya kuabudu miungu mingine,
Kumb 27:15 anasema "na alaaniwe mtu afanyae sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. na watu wote wajibu waseme Amina" Sasa kule kuabudu miungu mingine,au kuchonga kitu na kuanza kukisujudia, kunasababisha laana ya Mungu juu ya maisha yako.
{ b} Laana ya kuwadharau wazazi,
Wapo watu wanao wadharau wazazi wao, hawataki kufuata ushauri wa wazazi, na mbaya zaidi ni kule kuwadharau tu kwa sababu wao hawajaokoka, kumbuka Bado ni wazazi wako na bado wana baraka zako maana Mungu aliamuru waheshimiwe, Isipokuwa kama laana itatoka kwao bila sababu haitakupata wewe. Kutoka 20:12 waheshimu Baba yako na Mama yako; bila kujalisha wameokoka au hawajaokoka, matajiri au maskini, Mungu aliamuru waheshimiwe, sasa ukiendelea kidogo anasema "siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako." Sasa hii inaweza ikakusaidia kujua kuwa wako vijana wengi sana leo ambao hawakukubali kufunzwa na wazazi wao, kuwaheshimu wala kuwatii, wengi wao leo wameshapoteza maisha, isipokuwa wazazi, wakikutaka ufanye uovu, maana wapo pia, Mungu atakupa hekima ya namna ya kutokukubaliana nao. Na hata wakitaka kukulaani Biblia inasema laana isiyo sababu haimpati mtu.
{ c } Laana ya kufanya tendo la ndoa na dada yako au kaka yako
Kuna mambo mengine sio rahisi hata kuelezea lakini yapo na yanafanyika mtu amelala na Dada yake, mwingine na kaka yake, laana ya Mungu imeagizwa juu yao Kumb 27 :22 ‘na alaaniwe alalaye na Umbu lake, binti ya babaye au Binti ya mamae. Na watu wote waseme Amina .’
{d} Laana ya kutembea na mama yako au mke wa Baba yako.
Unaweza usielewe kuwa haya mambo yanafanyika sasa iyo ni laana ya Mungu juu ya mtu Kumb 27 :20 na alaaniwe alalaye na mke wa Baba yake,kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye na watu wote waseme Amina.
{e} Laana ya kumtegemea mwanadamu na sio Mungu
Wapo watu ambao wanawaheshimu Binadamu zaidi na kuwaogopa kwa kiwango cha kumpa Mungu nafasi ya pili kwenye maisha yao, Yeremia 17 :5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa amtegemeae mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amwemwacha Bwana. Mtu yoyote anaye mfanya mwanadamu kuwa kinga yake huwa anahesabiwa kuwa amemwacha Bwana, sasa ukiusoma ule mstali wa 6 anasema ‘maana atakuwa kama fukala nyikani, hataona yatakapotokea mema. Laana ya kumtegemea Binadamu zaidi na sio Mungu inakupa upofu ushindwe kuona tena baraka za Mungu kwenye maisha yako, maana tumaini lako limehamia kwa Mwanadamu.
{f} Laana ya udhulumaji
Kuna watu amabao wamewazulumu wengine, wamechukua sehemu ya ardhi ya wengine, pia wamechukua, sehemu ya mpaka wa nyumba ya mwingine na kudai sehemu hiyo ni yake na yuko teyeri hata kwenda mahakamani, lakini rohoni anashuhudiwa iyo sehemu si yake iko laana inaambatana na mtu huyu Kumbu 27 :17 ‘Na alaaniwe aondoae mpaka wa jirani yake’ Na watu wote waseme Amina, Na udhulumaji mwingine wowote mtu anao ufanya huwa unakuwa na laana nyumayake.
{g} Laana ya kuwakosesha walemavu
Wapo watu ambao hawawezi kabisa kusaidia vipofu hata akiona anakwenda kwenye miba, au mahali kusiko, wengine wanaona ni unajisi kuwasaidia vilema na wenye ukoma, sisemi ni lazima kuwasaidia isipo kuwa unapokuwa kwenye mazingira ya kumsaidia na ukamwacha katika hali ya kuhangaika inaleta shida Kumb 27 : 28 anasema ‘na alaaniwe ampotezae kipofu kukosa njia, na watu wote waseme Amina,’ anaposema ampotezae kipofu kukosa njia maana yake aliweza kumsaidia lakini akamwacha.
{h} Laana ya kumuibia Mungu zaka {fungu la kumi}
Watu wengi leo wamepandwa uongo na Ibilisi kuwa anapotoa sadaka inakwenda mahali fulani, fulani, na hivyo wanaacha kutoa fungu la kumi dhaka, ikiwa ni pamoja na sadaka zingine, kumbuka hapa sifundishi utoaji isipokuwa nataka tu ufahamu kuwa iko laana kwa wasiotoa, Maana Mungu anawahesabu kama wanao muibia, Maana ni bora ukatoa usijue unakokwenda maana nataka nikuambie Mungu ataipigania na kuifuatilia pesa yake, maana ni sadaka yake ambayo wewe umetoa, kulikoni kukoseshwa baraka zako,na hivyo kupata laana Malaki 3 :8 je mwanadamu atamwibia Mungu ? Lakini ninyi mnaniibia mimi. lakini ninyi mwasema, Tumemuibia kwa namna gani ? Mmeniibia dhaka na dhabihu. Sasa ukiusoma mstali wa 9 anasema ‘Ninyi mmelaaniwa kwa laana ; maana mnaniibia mimi….’
{i} Laana ya kupindisha injili
Wapo watu leo wangetamani hata kuibadilisha Biblia kama wangeweza, maana wanataka Biblia iwafuate wao wanavyotaka badala ya wao kulifuata neno la Mungu na kulitii, na ndio sababu kuna kitu kinaitwa manabii wa uongo, na wapotoaji wa maandiko, sasa kitu natamani ujue ni kuwa iko laana ya Mungu itakufuatilia tu endapo utapotoa maandiko na kuwapotosha wengine ukisoma Garatia 1 :6 anasema ‘Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya kristo, na kuigeukia injili ya namna nyingine, wala si nyigine lakini wapo watu wawatabishao na kutaka kuigeuza injiri ya kristo sasa mstali wa 8 anasema ‘Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubili ninyi injili yoyote isipokuwa iyo tuliyowahubiri na alaaniwe !’kitu nilitaka uone ni laana inayomkabili mtu yoyote anapopotoa injili ya kristo,
{j}Laana ya kuilaani Izraeli
Ndugu msomaji wapo watu wengi leo huisema vibaya Izraeli, bila kujua madhara yake, kwenye maisha yao, na matokeo yake laana kuwafuatilia bila ya wao kujua, ukisoma Mwanzo 12 :2 utakuta Mungu akimbariki Ibrahimu, na kumbuka kuwa katika ibrahimu alitokea Yakobo, ambaye baadae akaitwa Izraeli, na kwa Yakobo{Izraeli} tukapata kabira kumi na mbili za Izraeli, Taifa teule la Mungu ambalo ndilo tulilonalo mpaka sasa hivyo basi kama unataka kubarikiwa jifunze kuwabariki maana ukisoma Mwanzo 12 : 2 utaona Mungu akimwambia Ibrahimu anasema ‘nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako ; nawe uwe baraka ; mstari wa pili nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaanie nitamlaani ; na katika wewe jamaa zote za Dunia watabarikiwa. Sasa basi na wewe uko kwenye jamaa zote za dunia wanaotakiwa kubarikiwa endapo tu wataibariki Izraeli.

MOJA YA VITU VINAVYOWEZA KUKUASHIRIA MTU YUKO CHINI YA LAANA,VIFUNGO AU UNAFUATILIWA NA ROHO ZA GIZA:
Kuishi maisha ya kutokufanikiwa, kutokuvuka daraja fulani, kila unalojitahidi kulifanyia jitihada unaishia kuwa mtu wa kushindwa tu. Ziko familia amabazo hakuna mtu aliyewahi kuvuka level Fulani ya kimaisha. kama ni elim inaweza ikawa mwisho form four hakuna aliye wahi kuvuka hapo.hata kama mtu alikuwa anaakili vipi, anaishia kuvuta Bangi, na kupata mimba.
Kwa wengine mafanikio Fulani yanapotaka kutokea tu, ndipo linapotokea jambo la kurudisha nyuma, na anabaki kwenye ilo eneo siku zote. Misiba, magonjwa, ajali, na kutapeliwa
Maumivu yasiyo na sababu maalumu Mwili mzima, au Magonjwa ya ghafra na vipimo vya Hospitari kushindwa kuonyesha kitu chochote,
Wapo watu amabao huwa wanaota waliokufa mara kwa mara, wakati mwingine kuona unapaa hewani.
Kuota unakula au unalazimishwa kula nyama Fulani, wakati mwingine kuhisi kabisa ni za watu.au kuota unakimbizwa na majoka,wanyama wakali, mara kwa mara.
Tulifanya huduma na Binti mmoja Sumbawanga ambae Baba yake aliltaka alithi mikoba ya uchawi na yeye alikuwa hajui hilo, isipokuwa mara nyingi alimuona Bibi kizee katika ndoto aliyemtaka apokee mkoba wenye fifaa vya ushirikina, wakati mwingine alilazimishwa kula vitu Fulani.katika ndoto. Siku moja Baba yake akaja akamwambia wewe peke yako ndie uliyependwa na Bibi zako utatakiwa kushikilia mambo yetu ya mila na ntakufundisha namna ya kufanya. Ndipo yule binti akaelewa alichokuwa anakiona.
Wengine huwa wanaona wanadumbukizwa shimoni, analia kwa uchungu ukitafuta msaada.
Kupoteza ujasili, kuwa muoga kupita kiasi siku zote, kushindwa hata kukaa ndani peke yako, hasa wakati wa usiku.
Kuota unafukuzwa na waliokufa, au mnafanya nao vikao.
Kuota au kuona kwenye maono umevaa vifaa vya ushirikina kama Irizi,nguo za matambiko, na vikapu vyenye madawa ya kienyeji.
Wengine huona kama maono, au kuota kuwa wamelala juu ya Jeneza au makaburi .
Wapo wanao ota wamevaa mavazi ya kimila, wengine huota mara kwa mara wanaagua, au wapo kwa waganga wa kienyeji hata kama hajawahi kwenda.
Kusikia hisia Fulani Fulani ambazo si za kawaida mwilini kwa kipindi na kipindi, Wengine hupata mishtuko ya mara kwa mara na hawajui sababu, wengine huona mwili mzima unachomachoma, Vipindi Fulani Fulani.
Kutokushika kwa mimba, Au mimba kuharibika. Mara kwa mara.
Wengine huota wanafukua makaburi wakati mwingine wamebeba maiti za watu, na wakati mwingine umwagikaji wa Damu.na hivi vitu kutokea mara kwa mara, wakati mwingine unaona umebeba maiti na unashurutishwa kwenda nayo mahali Fulani. Hizo ni roho za giza
Kuishi maisha ya kukata tamaa siku zote, na kila wakati kufikilia ni bora kufa kuliko kuishi. Hizo ni roho za giza. Yesu alikataza kabisa kukata tamaa ila alitutaka tuishi maisha ya kuomba siku zote. "Luka 18:1 akawaambia mfano ya kwamba imewapasa kumuomba Mungu siku zote wala msikate tamaa."
Kuvunjika kwa ndoa na matengano kwenye familia.
Kusikia uchovu wakati wa ibada, miayo isiyo ya kawaida wakati wa maombi,
Kuwachukia watumishi wa Mungu bila sababu na kuwasema vibaya.
Kusikia sauti zisizo za kawaida zinazo ashiria hatari, {strange voices} vipindi Fulani, wengi husikia wakiwa kwenye ndoto. Wakati mwingine zinakuwa za watu waliokufa. Hizo zote ni roho za giza.
Uwezo wa kuona mambo ya kishirikina, kuona wachawi, kutoa unabii, kujua mambo ya watu wengine nje ya nguvu za Bwana Yesu. Mate 16:16 ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia Bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akasema watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Kitu nataka uone ni kuwa huyu kijakazi hakuwa na nguvu za Mungu isipokuwa za pepo na ilikuwa ni ngumu kujulikana ni mpaka Mungu alipomfunulia Paulo matari wa 18b Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule Pepo sio kujakazi tena Nakuamuru kwa jina la Yesu kristo, mtoke huyu, Akamtoka saa ileile. Lengo ni kukusaidia kuwa muangalifu maana si kila mtu anamuabudu Mungu aliyehai leo, na kutembea kwenye uweza na nguvu zake. Nakumbuka nikifanya huduma mahali Fulani nilikutana na mtu wa namna hii na watu wa eneo lile wote waliamini anatumia Nguvu za Mungu na kumbe ndani yake alikuwa na pepo lililo muwezesha kufanya mambo hayo yote lakini hata yeye alikuwa hajui, kwa Neema ya Mungu nilipata ufunuo juu ya ilo mara nilipomuona tu. Tulipofanya nae maombi tu nguvu za Giza zilimuachilia.kila mtu alishangaa.
Kuona unatembea kama nyoka kwenye ndoto, kuota ndoto za majoka, na mambo ya kishetani, pia mara kwa mara kuongea peke yako wakati uwapo usingizini, tena kwa mda mrefu.Ndugu msomaji nguvu za giza huweza kuwasiliana na mtu kwa njia ya sauti, ndoto na hisia. Na ndio maana unaweza kuhisi kwa kuongozwa na Roho mtakatifu kwa habari za uwepo wa nguvu za giza mahali, wakati mwingine hata zikiwa ndani ya mtu.Inawezekana haya yakawa yakitokea kwenye maisha yako lakini usiogope, Kumbuka kuwa kazi zote Yesu alimaliza pale msalabani Biblia inasema wazi kabisa kuwa udhihilisho wa Yesu Duniani ulikuwa ni kwa ajili ya kuzivunja kazi za Ibilisi. Ukisoma Yoh 3:8b "kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihilishwa azivunje kazi za Ibilisi. pia ukisoma {Kolosai 1:13} anasema "naye alituokoa katika nguvu za giza akatuamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake."
Ili mtu aweze kufunguliwa
Anahitaji utayari wa kuelezea mambo uliyowahi kufanya au kufanyiwa {making comfetional} hii ni kwa sababu uwazi unampa huyu mtumishi kujua namna ya kukupeleka mbele za Mungu.
Anahitaji kuwa na utayari wa kuviachia vitu ulivyovishikilia vile vya ushirikina inaweza ikawa ni mikoba ya uchawi au vitu vya aina yoyote ile, kutoka kwa waganga. Mfano wa vitu Irizi, vibuyu, mavazi ya aina Fulani, vitu vya kutambikia mizimu,Shanga za kuvaa, na kila aina ya kitu ulichopewa kwa ajili ya ushirikina, Ule utayari wa kuviachilia unafungua mirango ya uponyaji wako. Maana wapo watu wangependa kufunguliwa lakini bado wanataka kuendelea kushikilia hivyo vitu pia, wawe na uhakika hawata funguliwa maana Mungu awezi akamfungua mtu na kutaka aendelee na miungu mingine.
Vitu vya ushirikina amabvyo mtu hupewa vinamuunganisha yeye na falme za Adui {kuzimu} bila yeye kujua. Sasa basi mtu anapo amua kuachilia anakuwa ameamua kujitoa kwenye hicho kifungo kwa iyali yake mwenyewe,
Lengo ni kumsaidia mtu aifahamu kweli ya Mungu ili asiendelee kukubali manyanyaso ya Ibilisi Yoh 8:32 Nanyi mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru shida ni kuwa wapo watu wengi leo hata baada ya kuifahamu kweli bado wameendelea kuficha uovu wao na vitu vyao vya ushirikina japokuwa wanasali na Mungu wanampenda sana, wengine hufikili kuwa watu watanielewaje wakijuwa nilikuwa ninafanya haya, kumbuka ni kwa ajili ya ukombozi wako mwenyewe, ukishindwa kabisa fanya kama nikodemu utafanyiwa hata huduma ya ukombozi kwa siri.
Biblia imesema wazi kabisa "Mith 28:13 Afichae dhambi zake hatafanikiwa bali yeye aziungamae na kuziacha atapata rehema" Maana halisi ni kuwa mtu akificha kinachomtatiza hawezi kufunguliwa isipokuwa akiwa wazi zipo rehema za Mungu juu yake kwa ajili ya ukombozi wake.
WATU WALIOISHI CHINI YA VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA NA KUFUNGULIWA NA BWANA YESU
Yesu anamfungua mgerasi
Marko 5:1 wakafika ngambo ya bahari mpaka nchi ya wagerasi waliposhuka chomboni walikutana na mtu ambaye ametoka makaburini wala hakuna mtu yeyote aliyeweza kumfunga tena kwa minyororo, kitu nataka uone ni ni mateso na manyanyaso aliyokuwa nayo huyu mtu tu sababu tu ya nguvu za giza ukisoma mstari wa 5 utaona kitu kingine "na siku zote usiku na mchana alikuwako makaburini na milimani akipiga kelele na kujikata kata kwa mawe", sasa ukisoma kitabu cha Luka 8:27 utaona utaona huyu mtu akielezewa kwa kitu kingine, Biblia inasema " naye aliposhuka pwani yaani Yesu alikutana na mtu mmoja wa mji ule mwenye Pepo hakuvaa nguo siku nyingi wala hakukaa nyumbani" mapepo yalimshurutisha huyu mtu pia kutokuvaa nguo hapo nyuma kidogo tumeona yalimfanya asikae nyumbani,apige kelele, apende makaburini, ajikate kate kwa mawe.
Roho za giza zinatesa zichukie na kuzikataa kabisa kwa kuishi maisha ya kujilinda na maombi, nakumbuka tulifanya huduma na binti mmoja wa aina hii mkoa Fulani baada ya kufunguliwa alitupa ushuhuda jinsi amabvyo Roho za giza zilikuwa zikimuamuru kukaa uchi, watu walikuwa wakiondoka nyumbani anafunga mirango na kubaki uchi, wakirudi anajifungia chimbani kwake alieleza mambo mengi sana yaliyoambatana na hilo.
Yesu alipomfungua mwenye pepo kifafa
Math 17:14 "Nao walipoufikia mkutano mtu mmoja alimjia akapiga magoti akasema Bwana umreemu mwanangu kwa kuwa ana kifafa na kuteswa vibaya maana mara nyingi huanguka motoni na mara nyingi huanguka majini mstari wa 18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; Yule kijana akapona tangu saa ile,"
Nataka uone jinsi ambavyo yale mapepo yalikuwa yanamtesa huyu mtoto, hakuwa na amani wala furaha, maisha ya huyu mtoto yalijaa huzuni na mateso Biblia inaonyesha wazi jinsi amabavyo huyu mtoto alivyo angushwa motoni na majini,
Mi sijui kama ummewahi ona mtu wa hali hii tulipofanya huduma na mtu wa hali hii wkati Fulani nakumbuka alikuwa amejaa makovu, tulipouliza ni makovu ya nini walituambia jinsi amabavyo alikuwa akianguka motoni, na kwenye maeneo mengine mababaya, kumbuka sio mapenzi ya Mungu uishi hivyo hata kidogo. ELEWA WAZI KUWA MWANA WA MUNGU YESU ALIDHIHILISHWA APATE KUZIVUNJA KAZI ZA IBILISI, kwako binafsi,kwa mme wako,kwa watoto wako, kwa mke wako, na hata kwa wazazi wako.
Yesu alipo mfungua mwenye pepo la udhaifu
"uka 13:10 siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu mda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomuona alimwita, akamwambia, Mama umefunguliwa katika udhaifu wako, akaweka mkono juu yake naye akanyoka saa iyo, akamtukuza mngu. unaweza kuona kifungo cha huyu mama ilikuwa ni mgongo kupinda kwa mda wa miaka 18 japo sijui mamepo haya yalitaka yakae humo kwa mda gani, maana kama isingekuwa ni Yesu kumfungua huyu mama ni wazi kuwa yangeendea kukaa na kuendelea kumtesa huyu mama. Unapoendelea kufuatilia mafundisho haya endelea kutafakari ni kifungo gani kimekuwa kikikutesa kwa mda mrefu alafu amini Yesu yuleyule aliyeponya kipindi kile yuko teyari kukuponya na wewe leo, ukisoma Rumi 10:11 anasema " kwa maana andiko lanena kila amwaminiye hata tahayarika,…"
KWA MTU ALIYEOKOKA MAOMBI YA VITA NI MUHIMU KATIKA KUPINGANA NA HILA ZA ADUI.
Mtumishi wa Mungu mmoja nchini Marekani alizungumza hivi kwa lugha ya kiingereza ni maneno muhimu sana akasemaif thdevil has declared the war, we to declare the war against the devil" ikiwa na maana ikiwa shetani ametangaza vita, sisi nasi tunatangaza vita dhidi ya shetani, iko hivi kama Adui yako ametangaza vita dhidi yako hii ina maana amejiandaa, sasa wewe usipojipanga kukabiliana naye hii ina maana atakumaliza tu, lakini kama ukijipanga kwa vita, hata kama yeye ndiye aliye tangaza vita utamshinda tu. Ni muhimu ukafahamu kuwa shetani kila wakati anafanya vita na watoto wa Mungu. Lakini pamoja na hayo sisi ni washindi tunashinda na zaidi ya kushinda, "saya 42:13 Bwana atatokea kama shujaa ataamsha ataamsha wivu kama mtu wa vita,,,,,,,,,,,Atawatenda adui zake mambo makuu," Adui wa Bwana ni roho za giza zinazotesa na kusumbua maisha yako leo.
Maombi ya vita yakoje??
Ndugu mpendwa unayefuatilia mafundisho haya Maombi ya vita ni maombi ya kupambana katika ulimwengu war oho ukipambana na roho za giza, mapepo, na falme zote za giza
Aina hii ya maombi si aina ya tofauti na maombi mengine isipokuwa tu saa hii unakuwa katika hali ya vita ukikataa manyanyaso ya adui kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako, ukiamuru roho za giza kuachia maisha yako, watoto wako, mme wako, na hata biashara yako
Watu wengi waliokoka leo wangependa sana kuombewa, kitu amabacho ni chema isipokuwa unahakika gani kuwa unaombewa? Fikilia uko katikati ya maadaui na unategemea mtu mwingine awapige maadui kwa niaba yako na kwa sababu hajui uko kwenye hatari ya namna gani anaamua kufanya uzembe uwe na hakika utaangamia, hii ndio sababu ulipewa mamlaka dhidi ya nguvu zote za yule adui Math 10:1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu , wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina,
Ndani ya kila mtu aliyeokoka na anaye ishi maisha ya uaminifu mbele za Mungu, iko mamlaka na nguvu ya utiisho dhidi ya ibilisi na ndio sababu Biblia pia ikasema tutakayoyafunga Duniani yatakuwa yamefungwa na mbinguni, na tutayo yafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa na Mbinguni hii ina maana ndani ya mtu aliyeokoka kuna ufunguo wa kufungua mambo kwenye ulimwengu war oho,
Sasa watu wengi waliokoka leo hawana mda wa kukaa kwenye maombi na kupingana na na hila za adui kwenye maisha yao.
Na ndio sababu tunahamasisha mtu binafsi aliyeokoka kuwa na mda wa kupinga hila za shetani kwenye maisha yake kila inapoitwa siku, ukisoma katika Waefeso 6:10 anasema hatimae mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Sasa huwezi kuwa hodari katika Bwana kama huna mda wa maombi na kama huna mda wa maombi hii ina maana hauna ulinzi kwenye maisha yako maana ulinzi wa Mungu juu yako unategemea namna unavyopingana na adui kwenye maisha yako.na ukisoma mstari wa 11 utakuta anasema " vaeni siraha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani" sasa hii inakupa kujua kuwa kuna umuhimu wa kukaa kwenye maombi tena si kwa namna ya kawaida ili uweze kuzipinga hila za adui kwenye maisha yako,
Ukisoma mstari wa 12 utakuta anasema "maana kushindana kwetu si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wababaya katika ulimwengu wa roho"
Sasa unapoingia kwenye maombi ya vita ni kama askari anayeingia vitani, maana ni kwenye maombi haya ndiko ambako kuna kuamuru vitu Fulani vitokee au vizitokee, Yoeli 3:9-10 anasema " tangazeni haya kati ya mataifa takaseni vita, waamsheni mashujaa, watu wa vita na wakalibie na wapande juu yafueni majembe yenu iwe mikuki, aliye dhaifu na aseme, mimi hodari,
Maadamu umeokoka usijidharau amini tu kuwa kila unachokiamulu katika ulimwengu wa roho kwa mamlaka ya jina la Bwana kinatokea na ndia sabubu Biblia ikasema aliye dhaifu na aseme mimi hodari,
Maombi ya vita ni maombi ya kuvuruga mipango ya shetani kwenye maisha yako na familia yako hata taifa lako haya si maombi ya siku moja ni maombi ambayo unahitaji kufanya kila siku, maana ndani yake kuna ulinzi wa familia, kuna uponyaji wa ndoa, kuna ulinzi wa biashara yako na mambo mengine ambayo adui anayatafuta kwenye maisha yako kila siku.
Anayeomba maombi haya ni lazima awe ni yule anayeishi maisha matakatifu mbele za Mungu
Efeso 6:14 anasema Basi simameni hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa diriiya haki kifuani, jitahidi kuwa mtu wa kweli na mwenye haki mbele mbele za mungu sasa endelea na kufungiwa miguu utayari upatikanao kwa injiri ya amani zaidi ya yote mkitwaa ngao ya imani amabayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu
Hili ni jambo la muhimu kulielewa kuwa kila siku kuwa kunakuwa na mishale yenye moto toka kwa mwovu inayotumwa kwenye maisha yetu hivyo basi ni maombi tu ya kupingana na Adui kwenye maisha yetu ndio yaletayo msaadamstari wa 18 " kwa sara zote na maombi mkisali kila wakati katika roho, mkikesha kwa jambo hilo,,,,,,,"
Hivyo basi jifunze kuwa na muda maarumu wa kusogea mbele za Mungu kama askali wa vita kuhani na mfalme,ukijiweka wakfu kwa Bwana ukiweka wakfu nyumba yako,familia yako, na hata kazi yako.
Uwapo kwenye maombi haya amabayo ni mapambano kati yako na nguvu za giza tumia JINA LA YESU, DAMU YA YESU,
Ni muhimu kufanya yafuatayo kabla ya kufanya maaombi haya
Omba toba kwa Bwana ili kusiwe na ushitaki wowote wa adui juu yako, pata mda wa kujitakasa Isaya 1:16 jiosheni jitakaseni ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele ya macho yangu.
Usiingie kwenye maombi haya na hali unakinyongo na mtu moyoni hakikisha unasamehe "marko 11:26 lakini kama ninyi hamsamehee,wala baba yenu aliye mbinguni hata wasamehe ninyi makosa yenu."
Kumbuka haya ni maombi ya imani, amini tu kuwa unachokiamuru kwenye ulimwengu wa roho ndicho kinacho fanyika hata kama hauoni kwa macho Ebran 11:6 lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;yoyote amwendeae Mungu yapasa aamini ya kwamba Mungu yuko na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao
Pia imeandikwa katika kumbu 28:7 "Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yakowatakutokea kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba"
Hivyo basi iko namna maadui watakuwa wakishigulikiwa katika ulimwengu wa roho mara utapokuwa ukifanya maombi haya.
Futa kwa damu ua Yesu maneno mabaya uliyotamkiwa
Ni katika maombi haya unakotakiwa kufuta kwa damu ya Yesu kila aina ya maneno uliyotamkiwa futa maneno ya laana, mikosi, mabalaa, futa maneno mabaya kwa watoto wako kwa mke wako, kwa mme wako,
Futa kwa damu ya Yesu mambo mabaya ambayo hayataki kuiachilia nafsi yako, kunavitu uliwahi kuvisikia vikafanyika mzigo kwako, kunapicha uliwahi kuona, mapicha ya uchawi,mapicha mauti, mapicha ya uzinzi, futa kila kila kitu uwapo katika maombi haya.
Ni katika haya maombi unakoweza kukataa aina yoyote ya udhaifu iliyoko ndani yako bila msaada wa mtu mwingine ukaomba mwenyewe, ukapambana mwenyewe.
Mfano wako watu wanasumbuliwa na hofu ya mauti yaani kila wakati anaona yeye atakufa mda wowote ni roho tu ya adui ambayo ukijipanga kwenye maombi haya inakuachia, kataa kwa jina la Yesu tumia na damu ya Yesu zisomee roho za giza zab 118:17 "sintakufa bali nitaishi nami nitayasimulia matendo ya Bwana" kumbuka kibiblia siku zako za kuishi ni miaka 70 ukiwa na nguvu 80.
Ni katika maombi haya unaweza ukakataa magonjwa yanayoonekana kuutesa mwili wako wako tulifanya huduma na binti aliyekuwa akitokwa na damu maeneo ya siri kwa mda mrefu baadae tukagundua ilikuwa ni Roho za giza tu, badae tukagundua roho za giza zinasababisha mabinti wengine wasione siku zao, sasa yapo magonjwa mengine ni ya kawaida mengine sio ya kawaida ni katika maombi haya kila kitu kitu kinafanyika maana unapambana kwenye ulimwengu wa roho.Ni katika maombi haya unaweza ukakataa roho ya uchungu na hali ya kukataliwa
Ni katika maombi haya unaweza ukatakasa mavazi yako, vifaa vyako maana si kila tunachonunua Dukani au kwenye mtumba ni salama,
Pia maombi haya huzuia mapepo ya kulushiwa, Maana hakuna pepo litakalotumwa kwako na kufanikiwa.
Maisha ya maombi husababisha ulinzi na amani hata kama kuna roho za adui zinatenda kazi, Mambo ya walawi 26:6 nami nitawapa amani katika nchi tena mtalala wala hapana atakaye watia hofu……"
Hii ni mifano ya maombi ya vita
Jipangie muda inaweza kuwa Dakika 15 ukiwa na nguvu dakika 30 wapo wanaoweza kukaa kwa saa nzima, endapo unanena kwa lugha ni vizuri ukaomba pia kwa kunena kwa lugha.
Katika jina la Yesu, ninakataa kila aina ya mipango ya uharibifu wa shetani kwenye maisha yangu, manyanyaso na mateso,laana, mikosi, mabalaa, katika jina la Yesu, achieni maisha yangu, kwa Moto wa Roho mtakatifu, Nawaamuru ninyi roho za giza achieni baraka zangu, achieni uponyaji wangu, kwa Damu ya Yesu achieni maisha yangu, kila aina za roho za giza mnaosababisha mwili wangu ushindwe kutulia kwenye uwepo wa Mungu niachieni sasa, kwa kinywa changu ninawakana, hata kama mliwai kupata nafasi kwenye maisha yangu, leo ninawakana, na ninawasaliti, kwa jina la Yesu,
Kwa Damu ya Yesu ninajifunika, kwa mamlaka niliyopewa na Bwana Yesu, ninajitangazia baraka, kwa jina la Yesu nakataa hali yoyote ya kushindwa, kutokufanikiwa, najitangazia maisha marefu kwa jina la Yesu, najitangazia utajiri badala ya umasikini, kwa Jina la Yesu, maana neno la Bwana limesema aliyachukuwa masikitiko yetu, alifanyika masikini ili sisi tuwe matajili, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona kwa jina la Yesu ninajitangazia mafanikio na uwepo wa nguvu za Mungu maishani mwangu. Lihimidiwe jina la Bwana kwa sababu Bwana ameyatenda haya. Ameni
Wewe unaweza ukaomba mambo mengi zaidi hayo kwa kadri ya kiu yako na uhitaji wako omba mpaka uone kiu yako inaisha kulingana na muda wako uliojipangia.
Baada ya maombi haya amini, omba maombi ya aina hii kila siku, sasa aina hii ya maombi inaweza ikawa ni sehemu tu ya maombi yako unayoomba kila siku, aina maana uombe hivi tu kila siku, maana unahitaji kuombea mambo mengine.

FAIDA ZINAZOTOKANA NA MAOMBI YA VITA
Maombi haya yanazima mishale yenye moto toka kwa adui ambayo ingeelekezwa kwenye maisha yako, mishale yenye moto ni kama kusingiziwa, kuibiwa, kusimamishwa kazi bila sababu, kuchukiwa ofisini bila sababu yoyote, kuachwa na mchumba au arusi kuvurugika, ndoa kuvunjika, na yafananayo, hii yote ni mishale ya mwovu kwenye maisha yako sasa maombi ya vita huwa yanakwenda kwenye ulimwengu wa roho na kuizima hii mishale ya mwovu.
Roho za giza kushindwa kuvamia hata kama ziliamriwa kufanya hivyo, maombi haya hufunga ajali, huzuia mauti, ukisoma Mtend 12:5 basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamuomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake" haya hayakuwa maombi ya kawaida maana herode alikuwa amekwisha kumuua yakobo kwa upanga, kanisa likajua yamkini petro angefuata ndipo walipoamua kuingia kwenye maombi ya kuzima ile hila juu ya petro.Biblia inaonyesha wazi kuwa usiku ule ule malaika wa Bwana akashuka gerezani.
Ni kwa maombi haya vifungo mbalimbali vya adui huwa vinamwachia mtu na minyororo kufunguka kwenye maeneo mbali mbali ya maisha ikiwa anapata mda wa kuomba maombi haya.
Ni maombi haya amabayo yakielekezwa mahali yanasababisha watu waache pombe, sigara, ukahaba maana kuna watu walisimama kwenye ulimwengu wa roho kupingana na zile hila za adui kwenye maisha yao, na kungoa mizizi ya tamaa ikiwa ni pamoja na kuikata ile kiu ya pombe, sigara, ikiwa ni pamoja na tamaa mbaya.
Mara baada ya maombi haya watu hujisikia wepesi mwilini na hata katika ulimwengu waro pia Amani moyoni ikiashiria vifungo vimefunguka.

Naamini mpaka sasa Bwana atakuwa amefanya kitu kikubwa sana kwenye maisha yako, ikiwa ni ukombozi kwenye maeneo mbalimbali ya maisha, hivyo basi ingia kwenye maombi ya kumshukuru Mungu ukimwambia asente kwa ajili ya ufunuo aliokupa kupitia mafundisho haya,
Ndugu msomaji itakuwa ni vema endapo utapata nafasi ya kuniombea ukimsii Mungu anipe mafunuo zaidi, katika wito huu, anilinde na kunipa uzima ikiwa ni pamoja na kunifungulia mirango ya baraka.
Ombea mfululizo unaofuata wa masomo haya ujulikanao kama: Unavyoweza kuwa Mshindi dhidi ya mapambano tuliyonayo katika ulimwengu wa Roho.
Usisite kutuma ushuhuda wako
Kupitia mawasiliano yafuatayo
Mwl: Tuntufye Andew mwakyembe

Email tumsifu_Andrew@yahoo.com simu 0784 629562 na kwa uhitaji wa maombezi youth_ prayernet@yahoo.com pia C/o S.L.P 55 USA RIVER ARUSHA
ENDAPO UMEGUSWA NA HUDUMA HII NA UNGEPENDA KUPANDA MBEGU KWA KUSAIDIA KULIPIA SEHEMU YA GHARAMA
usisite kuwasiliana nasi.au waweza kutumia account No.016201033820 NBC.MBEYA BRANCH.
Kwa maelezo zaidi tumia Email ifuatayo yagotm28@yahoo.com