Saturday, May 31, 2008

TAMASHA LA INJILI KWA NAMNA YA PEKEE ARUSHA

Kuwashirikisha Christina Shusho, Frola Mbasha, Jackson Bent pamoja na Kwaya nyingine.

Waimbaji wa muziki wa injili Christina shusho na Frola mbasha toka Dar es Salaam wanatarajiwa
kuhudhuria katika tamasha la injili linaloandaliwa na IRPAYAN O’ NGERA ORGANIZATION ambalo ni shirika la dini linalohudumia watoto yatima mkoani Arusha.

Akizungumza na afu hii ya MAONI NA SALA, Muandaaji wa Tamasha hilo Bw.Jemsi Losioky alisema kuwa tamasha hilo litakuwa maalum kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi kwa matumaini wa kituo hicho.

Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika jumapili ya tarehe 8/06/2008 kuanzia saa nane mchana katika Hotel ya Gorden Rose jijini Arusha litapambwa na wakali wa injili hapa nchini ambaye ni Frola Mbasha na Christina Shusho kutoka Dar es Salaam.

Wengine ni Jackson Bent wa Arusha, Marther J. mushi, Sauti ya Nyikani Band wote kutoka Kilimanjaro pamoja na waimbaji wengine ambao hawakutajwa kwa sasa.

Tiketi za tamasha hilo kwa sasa zinapatikana kituo cha Radio ya Kikristo ya Safina FM iliyoko Arsuaha, Kimahama Bookshop pamoja na Golden Roze Hoteli (Arcade Comference Centre)

Tamasha hili linategemewa kuwa ni la aina yake kutokana na matamasha ya aina hii kutofanyika mara kwa mara.

Kwa mawasiliano zaidi 0754202623 au 0715 629562