Friday, May 30, 2008

SHUHUDA

Bwana asifiwe Mwl Tuntufye, pole na huduma, kitabu chako cha "SABABU 12 WATU KUKATA TAMAA KUIJERUHIKA NA KUPOTEZA MATUMAINI" kimenifanya nijione ninanafasi kubwa sana hapa duniani sikuwahi kujua hayo.
Nimefurahi sana najisikia huru mno Mungu akulinde na akufanikishe katika yote.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kwa Mungu kwa kazi unayoifanya maneno ya Mungu unayofundisha yamekuwa faraja kubwa sana kwangu kwangu.
Nikiwa nasoma kitabu ulichoandika kiitwacho "PAMBANA DHIDI YA NGUVU ZA GIZA" gafla nguvu za Mungu zilinishukia nikajikuta naanza kunena kwa Lugha, na kujaa nguvu za Mungu kwa mara ya kwanza, mpaka leo nafanya huduma za kuwaombea wenye nguvu za giza na nimesimama kiroho.

Mungu asifiwe ubarikiwe kwa ujumbe unaoutoa kwenye gazeti juu ya majaribu na kukata tamaa maana mara nyingi nilikuwa nikiwa katika hali hiyo naomba mniombee

Baada ya kusoma mafundisho mbalimbali aliandika hivi.
Nimefika hatua ya kuchoka natamani kulala katika kristo kwani nilianza na kristo toka utoto kila hatua nimemtegemea yeye amenionyesha baraka kubwa sana rohoni lakini mwilini sivioni ninampenda sana Yesu sasa ni zaidi ya miaka kumi kumi Moyo umechoka, nataka kuona mwilini la nilale nimechoka. Lakini Yesu alimsaidia.

Baada ya kusoma makala zenu kwenye gazeti na mafundisho kwenye vitabu nimepata nguvu za kusoma neno na kuomba Mungu awababriki sana
KARIBU NAWE UTUTUMIE USHUHUDA WAKO. KUPITIA MAWASILIANO YETU.