Monday, June 9, 2008

VITA VYA KIROHO

VITA VYA KIROHO
Efeso 6:12 kupigana kwetu si juu ya damu na nyama bali juu ya falme
Isaya 57:14 kila siraha itakayoinuka juu yako haitafanikiwa
2timoth 2:4 hakuna apigae vita ajitiae katiaka shughuli za dunia 7 Mungu hakutupa roho ya woga bali ya nguvu
Isaya 49:24 je aliye hodari aweza kupokonywa mateka yake?
Luka 10:19 nimewapa amri ya kukanyaga inge na nyoka na nguvu zote za yule adui
Efeso 3:20 kwa kadri ya nguvu itendayo kazi {neno li hai tena lina nguvu}
Ezekieli 22:30 nami nikatafuta mtu miongoni mwao {atakayepigana atakaye fight sikuona}
Zab 91:13 utawakanyaga samba na nyoka, mwanasimba na joka utawaseta chini ya miguu
Mith 24:10 ukizimia siku ya t

Aabu nguvu zako ni kidogo
Ayubu 22:28 nawe utakusudia neno nalo litathibitka kwako
2kor 10:3 ingawa tunaenenda katika mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili
1petro 5:8 mshitaki wenu kama samba anazunguka akitafuta mtu ammeze
Yoh 10:10 mwivi haji ila aibe na kuharibu mimi nalikuja ili wawe na uzima kasha wawe nao tele
Yer 11:10 nimekuweka juu ya mataifa na juu ya falme ili kungoa na kuharibu kujenga na kupanda
Yakobo 4:7mpingeni shetani nae atawakimbia
Efeso 4:27 msimpe ibilisi nafasi
Huwezi kuingingi akwa mwenye nguvu pasipo kuviteka vitu vyake

USHINDI DHIDI YA MAPAMBANO TULIYONAYO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
{VITAVYA KIROHO}
Ndugu yangu mpendwa ambaye Mungu kwa neema yake amekupa nafasi ya kufuatilia masomo haya yajulikanayo kama vita vya kiroho ninakusalimu kwa Jina la Yesu. Ni matumaini yangu kuwa Mungu kwa neema yake ameendelea kukutoa hatua kwa hatua, mara ulipoendelea kufuatilia masomo mbalimbali ambayo Roho mtakatifu amekuwa akitufundisha ni matumaini yangu kuwa Mungu kwa neema yake anakwenda kukufungua macho kwa namna nyingine tena utakapokuwa ukifuatilia ujumbe huu.
Ninapozungumza vita ya kiroho ninazungumzia suala la mapambano waliyonayo wateule dhidi ya roho za giza, Biblia inasema “Efeso 6:11 Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani,” hiki ni kitu muhimu sana mimi na wewe tunahitaji kukifahamu, kuwa maisha yetu yamezungukwa na hila za Adui, kwa masaa 24 kila siku, na Biblia imeweka wazi kabisa kuwa anatushitaki mbele za Mungu mchana na usiku, yaani wewe unapolala yeye alali maana ana kazi ya uharibifu yakufanya kwenye maisha yako “Ufunuo 12:10b kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu yeye awashitakie mbele za Mungu mchana na usiku”unapoendelea kusoma sura ya 12:12b Biblia inasema “Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akijua ana wakati mchahche tu”
Neno Ole maana yake inaweza kuwa onyo/angalizo, analopewa mtu ili aweze kuwa makini sana. Na mala nyingi huwa hili neno linatumika pale ambapo mbele huwa kunakuwa na hatari kubwa inayomkabali endapo hatakuwa muangalifu au endapo hatafuata kanuni fulani.
Na kwa sababu adui anatutafuta usiku na mchana apate kutuangamiza, hii ndio inayotulazimu kuvaa siraha zote za Mungu ili kila wakati tuweze kuzipinga hila za muovu. Kwenye maisha yetu, kwenye masomo yetu, kwenye ndoa zetu, kwa watoto wetu, wachungaji wetu, kwa wazazi wetu, kwenye safari zetu, na kila mahali tunapohitaji kuzipinga.
Ndugu mpendwa ni kitu cha kawaida kabisa kuwa, majumbani mwetu ama maofisini, au kwenye michezo, mahali popote tunapokuwepo, huwa tuanakuwa tumezungukwa na watu wenye misingi ya imani tofauti, tunakuwa tumezungukwa na wapagani, wachawi, wanaotumia na kumiliki Nguvu za giza, na wakati mwingine huwa tunakuwa tuna marafiki, Ndugu au watu wa jirani sana na sisi, wanaotegemea utatuzi wa matatizo yao yote kwenye uchawi, au kwa waganga wa kienyeji. Na wakati mwingine tunasafiri kwenye mabasi na Si rahisi kabisa kuwatambua watu wa mamna hii kwa macho ya nyama,
Hii ni muhimu sana kufahamu kuwa usipojua kuwa unahitaji kujipanga kila wakati kwenye maombi utaishi maisha ya hatari kila siku. Biblia inasema katika Efeso 6:10 hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.